Ndege zinazoangusha kinyesi angani kupigwa faini India
Image captionNdege zinazoangusha kinyesi angani kuigwa faini India
Ndege nchini India zitakazoangusha kinyesi cha binaadamu kutoka angani zitapigwa faini ya Rupee 50,000 sawa na dola 736 mahakama imeamuru.
Mtu mmoja amelalama kwamba ndege zimekuwa zikiangusha uchafu huo kutoka chooni juu ya makaazi ya watu karibu na uwanja wa ndege wa Delhi.
Vyoo vya ndege huweka uchafu wa chooni katika matangi maalum.
Matangi hayo hufunguliwa na uchafu huo kumwaga ndege inapotua.
Lakini mamlaka ya anga imekiri kwamba mtiririko wa uchafu huo hutokea angani kwa bahati mbaya.
Mahakama sasa imeagiza shirika hilo la usafiri wa ndege kuhakikisha kuwa kwamba ndege haziangushi kinyesi cha binaadamu kutoka anagani wakati inapotua ama mahala popte karibu na uwanja wa ndege
Boko Haram watimuliwa kutoka msitu wa Sambisa
Image captionWanajeshi wa Nigeria
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, anasema jeshi limeiteka kambi muhimu ya wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram iliyo msitu wa Sambisa.
Alisema kambi hiyo katika Msitu wa Sambisa, kaskazini-mashariki mwa nchi, ilitekwa siku mbili zilizopita.
Rais Buhari alisema Boko Haram sasa haina pahala pa kujificha, baada ya kutimuliwa kutoka maficho yake makubwa.
Katika miezi ya karibuni, jeshi limekomboa maeneo mengi yaliyo-dhibitiwa na wapiganaji hao; lakini bado wanafanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika nchi jirani za Niger na Cameroon.
Kumekuwa na uvumi kuwa baadhi wa wasichana wa Chikob ambao walitekwa nyara mwaka 2014 wanazuiliwa ndani ya msitu huo.
Baadhi ya wasichana waliofanikiwa kukimbia muda mfupi baada ya kutekwa nyara wanasema kuwa walikuwa wakishikiliwa eneo hilo.
Jeshi limetwaa maeneo kadha ambayo awali yalikuwa yakidhibitiwa na Boko Haram tangu harakati za kulishinda kundi hilo zianze.
Image copyrightGETTY IMAGESImage captionInaaminika kuwa baadhi ya wasichana waliotekwa walishikiliwa eneo hiloImage captionJeshi limetwaa maeneo kadha ambayo awali yalikuwa yakidhibitiwa na Boko Haram
Sunday, 11 December 2016
Zaidi ya 30 wafariki kwenye moto wa lori lenye gesi Kenya
Bonyeza 'EntIdadi ya watu waliofariki katika ajali mbaya ya kuteketea kwa lori nchini Kenya, imepanda na kupita watu 30.
Kwa mjibu wa naibu kamanda mkuu wa jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili katika eneo la Karai kwenye barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Naivasha.
Image copyrightREUTERSImage captionGari lililoteketea mjini Naivasha
Lori moja lilianguka na kulipuka katika eneo la barabara hiyo yenye shughuli nyingi nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu 30 papo hapo.
Watu wengine zaidi walifariki wakitibiwa mjini Naivasha.
Akihutubia waandishi wa habari hii leo, waziri wa masuala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery amesema kuwa watu 33 waliaga dunia wakimemo polisi 11 wa kikosi cha Recce ambacho humlinda rais na watu wengine mashuhuri.
Nkaisssery pia alisema kuwa sio gari la kusafirisha mafuta lililolipuka bali gari aina ya Canter lililokuwa na mitungi ya gesi inayoshika moto kwa haraka, iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Mombasa kwenda Kampala, Uganda,.
Image captionGari hilo lilikuwa limebeba kemikali
Mtu mmoja kwa jina Moses Nandalwe aliyeshuhudia ajali hiyo, ameiambia BBC kuwa, magari kadhaa yalishika moto na kuanza kuchomeka, huku watu wengi waliofika katika eneo la ajali hiyo ili kushuhudia kilichotokea, wakikumbwa na moto huo na kisha wakachomeka.
Image captionMlipuko huo wa lori ulitokea eneo la Naivasha lililo Kaskazini magharibi mwa Nairobi
Polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo. Kuna ripoti gari aina ya Canter iligonga tuta la barabarani na kisha kuyagonga magari yaliyokuwa yakitoka upande wa mbele kabla ya kulipuka.
Image captionAjali hiyo ilitokea karibu na mji wa Naivasha
Miongoni mwa magari yaliyoteketea ni Basi moja la matatu lililokuwa na abiria 14, ambao wanahofiwa wote wamefariki.
Ajali hiyo mbaya imetokea nchini Kenya, wakati ambapo madaktari na wauguzi wakiendelea na mgomo wao, hatua ambayo imelemaza kabisa shughuli za matibabu katika hospitali za umma.Idadi ya watu waliofariki katika ajali mbaya ya kuteketea kwa lori nchini Kenya, imepanda na kufikia 40
Thursday, 8 December 2016
Gumzo mtandaoni;Bibi awa mama Uingereza
Image captionJulie Bradford alibeba ujauzito kwa niaba ya bintiye Jesica
Ama kweli ,duniani kuna mambo!Mwanamke mmoja ameamua kubeba mimba, kuzaa mtoto kwa niaba ya bintiye.Mwanamke huyo jina lake ni Julie Bradford, mwenye umri wa miaka 45, alijifungua mtoto aitwaye Jack kwa niaba ya bintiye Jessica Jenkins, ambaye yuko katika matibabu ya ugonjwa wa saratani ambao umesababisha awe tasa.
Jessica, mwenye umri wa miaka 21, mwenyeji wa Rhymney, aliamua kupeleka mayai yake kugandishwa katika chuo kikuu cha utabibu cha Cardiff huko Wales kabla hajaanza matibabu yake ya saratani ya kizazi yalianza miaka mitatu iliyopita.
Jesica anasema tangu akiwa binti mdogo alikuwa na ndoto ya kuwa mama, na sasa ndoto yake imetimia, Jesica na mumewe Rees waliamua kutumia njia ya uzazi ya kupandikiza mapema mwaka huu.
Jesica aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani mnamo mwaka 2013, alipokuwa na umri wa miaka 18 wakati ambao madaktari waliona ni mapema mno kumuanzishia matibabu ya kansa ya kizazi .
Jesica anatoa ushuhuda kwamba madaktari walifanikiwa kuchukua mayai ishirini na moja tumboni mwake kabla ya kuanza matibabu na kati ya hayo ni mayai 10 ndiyo yaliyo nusurika yakaoteshwa kwa wiki mbili na baadaye kugandishwa, na mwezi wa tano mwaka huu yaliyeyushwa na kuwekwa tumboni mwa mamake Jesica na hivyo kumpa nafasi ya kuishi mtoto Jack na kukua tumboni mwa bibi yake.
Mamake Jesica anasema kwamba bintiye alipopewa taarifa za ugonjwa wake alijiona hana thamani tena na ndoto yake ya kuwa mama kuzimwa na saratani ya kizazi, wakati saratani ilipoondoa uwezekano wa Jess kubeba ujauzito wote tulikufa moyo.
Nikaamua kuwa nitabeba ujauzito kwa niaba yake na itakuwa fahari kuwabebea ujauzito kwa heshima ya familia ya mwanangu, tumetumia muda mwingi katika hospitali mbali mbali limekuwa jambo la kawaida kwetu. Nina furaha ya ajabu kwamba mara hii imekuwa kwa sababu maalum.
Waliomlazimisha mwafrika kuingia jeneza wanyimwa dhamana Afrika Kusini
Wakulima wawili wazungu nchini Afrika kusini wanaolaumiwa kwa kumlazimisha mwanamme mwafrika kuingia kwenye jeneza kwa kupitita shamba lao wamenyimwa dhamana na mahakama.
Mwezi uliopita Theo Martins Jackson na Willem Oosthuizen, walifunguliwa mashtaka ya kuteka nyara na kudhuluma kwa viwango vya kusababisha madhara ya kimwili.
Walikamatwa baada ya video moja ya dakika ishirini ambayo ilirekodiwa tarehe 17 mwezi Agosti kuanza kusambaa mitandaoni ikionyesha mwanamme mzungu akimlazimisha mwanamme mwafrika kuingia kwenye jeneza, akimtishia kumumwagia mafuta na kumchoma.
Taarifa zinasema kuwa mwendesha mashtaka alipinga wawili hao kuachuliwa kwa dhamana akidai kuwa muathiriwa Victor Mlotshwa ametishiwa maisha tangu akamatwe.
Jaji anayesikiliza kesi ametaja kitendo hicho kuwa cha kushangaza na cha kibaguzi na kuongeza kuwa si jambo la kushangaza kuwa ulimwengi ulishtushwa nacho
Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dk Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
ADVERTISEMENT
By Colnely Joseph,Mwananchi cjoseph@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Dk Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina nafasi aliyokuwa nayo Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine; pia amemteua Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dk Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.
Pamoja na mabadiliko hayo ya Singida, kadhalika Rais amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo.
Amemteua Profesa Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. Profesa Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.
Kadhalika Rais amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mtigumwe anachukua nafasi ya Dk Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Pmamoja na Turuka, Rais Magufuli amemteua Dk Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano atakayeshughulikia Mawasiliano.
Dk Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.
Wengine walioteulwia ni Mhandisi Angelina Madete anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Sasabo.
Aloyce K. Nzuki ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.