Friday, 20 January 2017

BREAKING NEWS: Yahya Jammeh apewa masaa ya mwisho(GAMBIA)

Kusherehekea Adama Barrow mjini Banjul, 19 Januari 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHabari za kuapishwa kwa Adama Barrow zilipokelewa kwa furaha na shangwe Banjul

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi wa Senegal wakiingia nchini Gambia.
Bw Jammeh amepewa hadi saa sita mchana Ijumaa (saa tisa Afrika Mashariki) kuachia madaraka la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi hao wametakiwa kusubiri hadi makataa hayo yamalizike.
Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) inaunga mkono Adama Barrow, ambaye aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo nchini Senegal.
Juhudi za mwisho za kumshawishi Bw Jammeh kuondoka kwa hiari, ambazo zinaongozwa na Rais wa Guinea Alpha Conde, zinatarajiwa kufanyika Ijumaa asubuhi.
Mwenyekiti wa tume ya Ecowas, Marcel Alain de Souza, alisema iwapo mkutano huo utakaoongozwa na Bw Conde hautafaulu, basi hatua ya kijeshi itafuata.
"Iwapo kufikia saa sita mchana, yeye (Bw Jammeh) hatakubali kuondoka Gambia chini ya Rais Conde, tutaingilia kijeshi," amesema.

Adama BarrowHaki miliki ya pichaRTS
Image captionAdama Barrow baada ya kuapishwa aliwaamuru wanajeshi wa Gambia wasalie kambini

Wanajeshi wa Ecowas walisema hawakukumbana na pingamizi zozote kutoka kwa wanajeshi wa Gambia walipoingia nchini humo Alhamisi baada ya kuapishwa kwa Barrow.

Wanajeshi kutoka Senegal na nchi nyingine za Afrika Magharibi waliingia Gambia baada ya makataa mengine aliyopewa Bw Jammeh kuondoka kumalizika.
Bw Jammeh, ambaye bado yupo nchini Senegal amesema hatarejea mji mkuu wa Gambia, Banjul, hadi operesheni ya kijeshi imalizike.
Hatua ya Ecowas kutaka kumtoa kwa nguvu Jammeh inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15, ingawa baraza hilo lilisisitiza kwamba suluhu ya amani inafaa kupoewa kipaumbele.

SenegalHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Senegal ni miongoni mwa waliopokea mafunzo zaidi Afrika

Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye, aliambia BBC kwamba wanajeshi wa Senegal tayari wamo nchini Gambia na wamejiandaa kupigana hali ikibidi.
"Tayari hivi ni vita, tukikumbana na upinzani wowote, tutapigana," amesema, na kuongeza: "Iwapo kuna watu wanampigania rais huyo wa zamani, tutapigana nao."
Lakini Kanali Ndiaye alisema lengo kuu la Ecowas ni kurejesha demokrasia na kumruhusu rais huyo mpya kuchukua hatamu.
Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa mjini Dakar, Rais Barrow aliwaamuru wanajeshi wanajeshi kusalia kambini.
Alisema wanajeshi watakaopatikana wakiwa na silaha nje ya kambi watachukuliwa kuwa "waasi."

Mbona Jammeh hataki kuondoka madarakani?

Jammeh anataka uchaguzi mpya ufanyike GambiaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJammeh anataka uchaguzi mpya ufanyike Gambia

Bw Jammeh awali alikubali kwamba Bw Barrow alishinda uchaguzi lakini baadaye akabadili msimamo wake na kusema hangeachia madaraka.
Alitangaza hali ya tahadhari ya siku 90 na kuhimiza "amani, utulivu na kufuatwa kwa sheria" baada ya kile alichosema ni udanganyifu uchaguzini.
Alisema tume ya uchaguzi ilifanya makosa mengi, na baadhi ya wafuasi wake walizuiwa kupiga kura vituoni.
Tume hiyo baadaye ilikubali kwamba baadhi ya matokeo yaliyotangazwa yalikuwa na makosa, lakini ikasema makosa hayo hayangeathiri ushindi wa Bw Barrow.
Bw Jammeh amesema atasalia madarakani hadi uchaguzi mpya ufanyike.
Hatua yake ya kuendelea kung'ang'ania madaraka itahakikisha kwamba hashtakiwi kutokana na makosa aliyoyatenda wakati wa utawala wake.
Mbona Senegal inaongoza kumkabili
Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.
Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh makataa ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.

Map of The Gambia

Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.
Hii inaifanya vigumu kufikiria ni vipi wanaweza kuwashinda wanajeshi wa kanda hiyo, anasema mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo.
Nigeria imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.
Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.
Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.

Sunday, 8 January 2017

19 Things All Couples Should Do More of in 2017

There are plenty of things you can do to improve your relationship in the long run, but you can also give it a boost right now. By focusing on the small, intimate moments, you can quickly strengthen your connection and turn up the heat. Looking for simple ways to feel closer to your other half? Keep reading for a look at easy tips to give your relationship an instant boost, then check out signs you've found your soul mate plus fun things to do with your partner this Summer.
  1. Send a flirty text.
  2. Bring up an old, awesome memory your other half may have forgotten.
  3. Hop in the shower together.
  4. Order a book for your SO just because.
  5. Plan your next vacation together.
  6. Have sex.(to who married)
  7. Have phone communication.
  8. Teach each other how to do something the other doesn't know how to do.
  9. Turn on "your song."
  10. Get nostalgic and pull up a photo from your early days together.
  11. Give each other massages.
  12. Go for a walk together (and turn of your phones.)
  13. Collaborate on a dating bucket list.
  14. Build a fort in your living room.
  15. Look through old photos from the early days of your relationship.
  16. Write each other love letters and actually mail them.
  17. Find out what your love languages are and compare notes.
  18. Read the first pages of your favorite book to your other half.
  19. Share stories you've never told each other.

Saturday, 24 December 2016

Tunisia yamkamata mpwa wa mshambuliaji wa Berlin

IS walitoa kanda ya video ikimuonyesha Amri akilitii kundi hiloImage copyright
Image captionIS walitoa kanda ya video ikimuonyesha Amri akilitii kundi hilo
Vikosi vya usalama nchini Tunisia vimemkamata mpwa wa mshambuliaji kwenye soko mjini Berplin, Anis Amri na washukiw wengine wawili.
Wizara ya masuala ya ndani nchini Tunisia, inasema kuwa watu hao wenye umri kati ya miaka 18 na 27 ni wanachama cha kundi la kigaidi.
Mzaliwa wa Tunisia Amri, mwenye umri wa miaka 24, aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi karibu na mji wa Milan nchini Italia mapema Ijumaa.
Shambulizi la lori la siku ya Jumamosi kwenye soko, lilisababisha vifo vya watu 12 na kuwajeruhi wengine 49.
Wizara ya masuala ya ndania ilisema kuwa mpwake huyo Amri, alikiri kuwasiana na mjombake kupitia mtandoa wa Telegram ili kukwepa kuchunguzwa.
Inaripotiwa kuwa watatu hao wemekuwa wakihudumu kwenye miji ya Fouchana nje ya mji wa Tunis na Oueslatia karibu na nyumbani kwao Amri, umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu.

JEFF HABARI BLOG ;TUNAWATAKIA CHRISTMAS NJEMA NA  HERI YA MPYA.

HUYU NI MMILIKI WA BLOGI AKIWATAKIA HERI YA SIKUKUU.

Katika msimu huu wa sikukuu tunawakaribisha wateja wetu kutoa matangazo kupitia blogi yetu hii kwa bei nafuu ili yawafikie watu wengi zaidi kwa muda mfupi zaidi.Tangaza nasi kukuza biashara yako hapa..

Ujauzito hubadilisha ubongo wa mwanamke

Mwanamke mwenye mimbaImage copyrightTHINKSTOCK
Image captionKiwango cha homoni huongezeka sana mwanamke akiwa na mimba

Wanasayansi wanasema kuwa mjamzito hubadilisha ubongo wa mwanamke, kwa kipindi cha hadi miaka miwili.
Wanasema uja uzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi ya sehemu za ubongo wa mwanamke, ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi na mtoto na kujiandaa kwa majukumu yake kama mama.
Uchunguzi ulifanyiwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo.
Lakini hata hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka kumbukumbu.
Wanawake wengi husema huwa wanajihisi kuwa wasahaulivu na kuwa wepesi wa kuekwa na hisia wakati wanabeba mimba.
Mara nyingi huwa wanalaumu kilichobandikwa kuwa ubongo wa "uja uzito" au "mtoto".

Ongezeko la homoni

Mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen huongezekana sana na pia mwili wake kubadilika, watafiti wanasema.
Hata hivyo, si wataalamu wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.
Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na Leiden walichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye ubongo.
Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience.

Mwanamke na mtotoImage copyrightTHINKSTOCK
Image captionMabadiliko hayo kwenye ubongo yanaaminika kuwaandaa wanawake kuwa na uhusiano mwema na watoto wao

Walilinganisha mabadiliko hao kwenye ubongo wa wanawake na ubongo wa wanaume 19 waliokuwa wamekuwa baba mara ya kwanza,wanaume 17 ambao hawakuwa na watoto na wanawake 20 ambao hawajawahi kujaliwa watoto.
Walishuhudia kupungua sana kwa seli za ubongo katika maeneo ambayo hutumiwa na ubongo katika kuhusiana na watu wengine.
Watafiti wanasema mabadiliko hayo huenda ni ya kuwafaa wanawake kwa njia kadhaa zikiwemo - kuwawezesha kupangia mahitaji ya watoto wao, kuwa na ufahamu zaidi kuhusu hatari kwa watoto wao kutoka kwa jamii na pia kuwawezesha kuhusiana zaidi na watoto wao