- Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mp
- Sambaza habari hii Faceboo
- Sambaza habari hii Twitter
- Sambaza habari hii Messenge
- Sambaza habari hii EmailMshirikishe mwenzako
TUNAKUPATIA HABARI ZA BIASHARA MICHEZO AFYA SIASA NA BURUDANI NA MAHUSIANO TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KUPITIA 0657191827,0753127275,0789930603
Friday, 19 May 2017
Sunday, 7 May 2017
Wanafunzi 32 wafariki katika ajali Arusha, Tanzania

Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha.
Mkasa huo umetokea takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ,takriban kilomita 150 kutoka mji wa Arusha.
Wanafunzi hao walikuwa wamesalia na kilomita 5 ili kufika sehemu waliokuwa wakielekea.

Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwalimu ilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi na waalimu wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano.
Mwandishi wa BBC mjini Arusha Ally Shemdoe, aliyeko mkoani humo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mvua kali inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.
- Watu kadha wafa kwenye ajali ya mashua Tanzania
- Takriban watu 9 wanahofiwa kufa maji visiwani Zanzibar
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa Tanzania
Anasema kwamba dereva alidaiwa kutoijua barabara hiyo hivyobasi alikosa mweleko na kuteleza kando ya barabara kabla ya kutumbukia korongoni katika mto Malera.

Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.
Shule hizo mbili zimekuwa zikifanya utaratibu wao wa kawaida,
Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa muujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , ni kuwa maiti zilizopokelewa katika hospitali hiyo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu wawili, dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa.
Kati ya wanafunzi waliopoteza maisha yao 10 ni wa kiume huku 18 wakiwa wasichana.
Aidha maiti zitahifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.
Mkuu wa wilaya ya Arusha , Fabian Dagalo amewataka wananchi kuwa watulivu kutokana na tukio hilo baya, na kwamba serikali itatoa taarifa baadaye kuhusiana na msiba huo
Friday, 5 May 2017
IJUE NGUVU YA SADAKA NA KUMBUKA KUMTOLEA MUNGU

Neno SADAKA ni neno ambalo si geni masikioni mwa watu wengi na lina maana nyingi sana, nitatoa maana kama tatu hivi za neno sadaka. Na zipo aina nyingi za sadaka kuna fungu la kumi, limbuko , sadaka ya shukrani na nk. Leo tutaangali sadaka kwa ujumla, Nguvu ya sadaka unapotoa katika Uwepo wa Mungu
Sadaka ni sehemu moja wapo ya kumuabudu Mungu, mwanzo 22:5 "Ibrahimu akawaambia vijana wake , kaeni hapa pamoja na punda , na mimi na kijana tutakwenda kule TUKAABUDU na kuwarudia tena"
Sadaka ni "kuonyesha upendo wako kwa Mungu" au unaweza kusema Sadaka ni "ushirika wetu katika kazi ya Mungu"
Mungu aliweza kurudisha majira mapya katika nchi baada ya Nuhu kutoa sadaka. Hatuoni mahali ambapo Mungu amemuangizia/amemwambia Nuhu atoe sadaka au atengeneze madhabahu kwa ajili ya kumtolea Mungu sadaka kama alivyokuwa akiwaangiza baadhi ya watumishi wengine mfano: Musa aliagizwa awaambie wana wa Israel watoe sadaka au Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka.
Swali la kujiuliza ni kitu gani kilimfanya Nuhu amtolee Bwana sadaka? Hatuoni Mungu akiongea na Nuhu baada ya kutoka ndani ya safina na wala biblia haituambi Nuhu alichukua muda gani tangu atoke ndani ya safina Mungu aliongea naye tena, inachotuambia ni Nuhu mara baada ya kutoka ndani ya safina alimjenge Bwana madhabahu na kumtolea sadaka ya kuteketezwa na iliyompelekea Mungu kufanya jambo jipya, Mungu anarudisha majira mapya katika nchi, na kumpa kutawala na kumiliki juu ya vitu vyote vya dunia hii yeye pamoja na watoto wake Nuhu.
Kuna kitu lazima ujifunze wakati mwingine unashindwa kupokea Baraka zako kwanini,kwasababu haumtolei Mungu katika kiwango kinachompendeza na mahali ambapo hapana uwepo wake,Watu wengi tumetoa sadaka zetu katika hali ya mazoea,desturi na taratibu za ibada,kujilazimisha wakati mwingine hata kutaka kuonekana na watu unashindwa kuelewa nguvu iliyopo ndania ya sadaka? kwasababu unapotoa sadaka pasipo uwepo wa Mungu mahali hapo ujue sadaka yako haitaleta majibu ila ukitoa sadaka yako mahali ambapo kuna uwepo wa Mungu huwa majibu hayachelewi mfano kwa Nuhu, Ibrahimu
Tunaona katika mwanzo 8:21-22 Mungu amesikia harufu nzuri ya sadaka ya Nuhu ambayo hiyo sadaka imemlazimisha Mungu ajisemeshe(ajiapize) mwenyewe moyoni mwake au kwa lugha nyingine tunaweza kusema sadaka ya Nuhu ilimlazimisha Mungu kufanya kitu hata kama Mungu hakukipanga kukifanya.
Mwanzo 8:21b “WALA SITAIPIGA TENA BAADA YA HAYO KILA KILICHO HAI KAMA NILIVYOFANYA SITAILAANI NCHI……” Kutokana na andiko la mwanzo Mungu anaposema sitailaani nchi kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mungu alikuwa na kawaida ya kuilaani nchi au kuna laana iliyokuwa inakuja mbele kwa ajili ya nchi kutomsaidi kwa kitu chochote atakachokifanya juu yake, ila kwa ajili ya na sadaka ya Nuhu, Mungu alijiapiza mwenyewe moyoni kuwa hatafanya hivyo tena, na anaposema TENA maana yake milele hakitakuwepo au hakitajirudia. Kwahiyo sadaka inanguvu ya kubadilisha kitu chochote unachokitaka na ndio maana wapo watu wanaoenda kwa waganga kwa ajili ya kutaka utajiri hivyo ilawazimu kutoa sadaka sawasawa na mganga aliyowaangiza ili kupata kitu wanachokitaka.
Jifunze kumtolea Mungu sadaka hata kama uliyokuwa nayo ni kidogo kwa kiasi gani au kinauhitaji mkubwa kwa wakati huo ili Mungu ajue na kukuamini katika kitu kidogo na chenye umuhimu kwako wewe hukumyima Mungu na ukamfanya kuwa wa kwanza katika yote kuliko hitaji lako ndipo malaki 3:10 itakapotimia kwako.
Monday, 1 May 2017
Monday, 24 April 2017
Wednesday, 12 April 2017
Saturday, 25 March 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)