TUNAKUPATIA HABARI ZA BIASHARA MICHEZO AFYA SIASA NA BURUDANI NA MAHUSIANO TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KUPITIA 0657191827,0753127275,0789930603
Sunday, 3 December 2017
Monday, 30 October 2017
BREAKING NEWS MBUNGE WA SINGIDA KASKAZINI RAZARO NYARANDU AJIUZURU NA KUOMBA KUHAMIA CHADEMA.
NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.
VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.
HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM
HISTORIA YAKE:
Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida.
Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987. Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 – 1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.
Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari, Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (Ukwata) 1991 – 1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro, Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.
Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.
Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo. Kiongozi huyu, sasa ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.
Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni, Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West, akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.
Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, China na nyinginezo. Pia, alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na k
I
Wednesday, 4 October 2017
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU 2017/2018
Sunday, 17 September 2017
BREAKING NEWS *NACTE ; MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KATIKA VYUO VYA AFYA NA UALIMU VYA SERIKALI 2017/18
BREAKING NEWS *NACTE ; MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KATIKA VYUO VYA AFYA NA UALIMU VYA SERIKALI 2017/18* NACTE Imetangaza kumalizika kwa Uhakiki wa Udahili wa Wanafunzi wanaotarajia kujiunga kwenye vyuo vya Serikali, Afya na Ualimu , Unaweza kuangalia matokeo ya Selection kwa kubofya kwenye linki hapo👇👉👉http://www.tzjobconnection.com/2017/09/nacte-diploma-and-certificate-selection.html
*http://www.tzjobconnection.com/2017/09/nacte-diploma-and-certificate-selection.html
Friday, 15 September 2017
Tanzania yashangazwa na uchunguzi wa UN kuhusu Korea Kaskazini

Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Tanzania
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, waziri wa mambo ya nje Dkt. Augustine Mahiga, amesema licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mnamo mwaka 2014, Tanzania imepunguza kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.
"Hatuna ugomvi na Korea Kaskazini,lakini kitendo chao cha kutengeneza masilaha ya kuangamiza sio mazuri kwa heshima na usalama duniani.Ndiyo maana tukaanza kuchukua hizo hatua za kupunguza mahusiano." amesema Dr Mahiga kwa waandishi wa habari leo.
Waziri Mahiga ameongeza kusema kuwa, uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa.
Waziri huyo amesema anaelekea katika mkutano wa kawaida wa Umoja wa Mataifa, ambapo atatumia fursa hiyo kujibu tuhuma hizo kwa Baraza la Usalama.
Tanzania na Uganda ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazochunguzwa na Umoja wa Matiafa kwa tuhuma za kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Ripoti ya uchunguzi huo ilitolewa mnamo tarehe 9 mwezi wa Septemba. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linachunguza tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini inayogharimu dola za kimarekani milioni 12.5
Subscribe to:
Posts (Atom)