Thursday, 23 February 2017


Korea Kaskazini yasema China ni kibaraka wa Marekani

Korea Kaskazini waishutumu china kwa kuwa kibaraka wa Marekani
Image captionKorea Kaskazini waishutumu china kwa kuwa kibaraka wa Marekani
Korea kaskazini imemshtumu mshirika wake wa kimataifa China ikimtuhumu kwa kukubali matakwa ya Marekani.
Wiki iliopita China ilitangaza marufuku ya kununua makaa kutoka Korea Kaskazini ikijibu hatua ya taifa hilo ya kufanyia majaribio ya makombora ya masafa marefu.
Taarifa hiyo haikuitaja China lakini ilisema kuwa taifa jirani linalojidai kuwa rafiki.
Hili taifa ambalo lina uwezo mkubwa limeanza kutii matakwa ya Marekani, kilisema chombo cha habari cha taifa hilo.
Ikizungumzia moja kwa moja kuhusu marufuku ya biashara ya kigeni, taarifa hiyo ilisema kuwa China imechukua hatua isiokuwa ya kibinaadamu kama vile kusitisha biashara ya kimataifa ambayo itawasaidia maadui zake kudhoofisha mpango wa kijamii wa Korea Kaskazini.
Taifa hilo linategemea sana biashara yake ya makaa na China kuingiza fedha za kigeni

No comments: