TUNAKUPATIA HABARI ZA BIASHARA MICHEZO AFYA SIASA NA BURUDANI NA MAHUSIANO TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KUPITIA 0657191827,0753127275,0789930603
Thursday, 7 December 2017
KISA CHA KUSISIMUA
Nakumbuka enzi hizo nikiwa mtoto mdogo nilikua na tabia ya kuchezea mawe kwa kuyarusha huku na huko.
Siku moja nilirusha jiwe likampata kuku wetu na kufariki palepale. Mama alikuwa akimhusudu sana yule kuku. Kwani alikuwa akitaga mayai mengi sana.
.
Wakati jiwe lilipompata yule kuku na kumuua palepale nilifikiri nilikuwa peke yangu katika mazingira yale. Kumbe dada yangu alikuwa upenuni mwa nyumba yetu akishuhudia jinsi nilivyomuua yule kuku.
.
Hivyo akaniambia, "Deo nimeona ulivyomuua kuku sasa nipe shilingi 50 vinginevyo nitamueleza mama kwamba ni wewe ndiye uliyemuua kuku wake."
.
Nikamwambia "Dada mi kwa sasa sina hiyo hela, tafadhali usimwambie mama, atanichapa kweli"
.
Siku iliyofuata, mama akamwambia dada yangu aoshe vyombo na kufagia uani, ila dada akamwambia mama: "Mama, Deo amesema atafanya usafi na kuosha vyombo yeye."
Halafu akaja kwangu na kuniambia: "Deo, osha vyombo na kufagia uani vinginevyo nitamwambia mama kwamba umemuua kuku wake". Bila kupinga nikaenda kuosha vyombo na kufagia.
.
Siku iliyofuata, mama alimwambia dada yangu aende kuteka maji kisimani na kujaza jaba. Akamwambia mama tena: "Mama, Deo amesema atachota na kujaza peke yake"
.
Hakafu akaja kwangu na kuniambua: "Deo, unamkumbuka yuke kuku uliyemuua? Jaza maji jaba ama sivyo nimueleze mama kwamba wewe ndiye uliyemuua kuku wake..." Hivyo nikajikongoja kuchota maji 'trip' za kutosha mpaka nikajaza jaba.
.
Siku hiyo hiyo jioni nikiwa nimechoka kweli, mama akamtuma dada aende sokoni kununua viazi na mahitaji mengine. Kwa mara nyingine tena akamwambia mama: "Deo amesema anahamu ya kwenda sokoni, anaomba aende yeye kununua."
.
Akaja kangu tena na kunuambia: "Deo, usisahau kuwa kuku bado amekufa, nenda sokoni na ununue viazi na mahitaji haya mengine, vinginevyo...."
Nilichoka!! Nilisimama na kwenda kwa mama huku machozi yakibubujika machoni mwangu, nikamkuta akiwa amekaa akisuka ukiri, nikamfuata na kupiga magoti mikono nimeifumba usawa wa kifua changu huku nikilia nikamwambia;
"Mama, nisamehe mimi. Mimi ndiye niliyemuua kuku wako ila haikuwa makusudi ni bahati mbaya tu katika kucheza kwangu, tafadhali sana mama nisamehe mimi."
.
Mama akanijibu huku akininyanyua: "Mwanangu ile siku umemuua kuku, nilikuwa dirishani nikiangalia kila kilichotokea. Dada yako alikufanya mtumwa wake kwa sababu hukutaka kuja kukiri kosa na kuomba masamaha."
"Lakini kwa kuwa umeona unateseka umekuja kukiri na kuomba msamaha, uko huru sasa, hatakutumikisha tena"
∆
Maana ya yote hayo ni nini?
Kila mara tunavyotenda dhambi, Mungu anatuona na dhambi hizo zinatufanya tuwe watumwa. Kipindi ambacho tutakiri dhambi zetu na kutubu kwa muumba wetu basi atatuweka huru na tutaishi kwa amani, furaha na kheri.
Basi Mwenyezi Mungu atujalie tuwe na moyo wa toba ya kweli pale tunapokengeuka...Amen!
Comment na SHARE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment