Wednesday, 28 March 2018

Ureno 0-3 Uholanzi: Cristiano Ronaldo apigwa breki mjini Geneva

 


Cristiano RonaldoHaki miliki ya pichaEPA

Mabingwa wa Ulaya Ureno walipokezwa kichapo cha kushangaza na Uholanzi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezewa mjini Geneva, Uswizi.
Winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Ryan Babel waliwaweka Waholanzi 2-0 mbele.
Beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ambaye majuzi alitawazwa nahodha mpya wa timu hiyo, alifunga la tatu.
Mchezaji wa Ureno Joao Cancelo alipewa kadi nyekundu dakika ya 61 baada ya kupokezwa kadi ya pili ya manjano.

Cristiano RonaldoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCristiano Ronaldo alikuwa amefunga mabao mechi nane mfululizo kabla ya mechi hiyo

Katika mechi hiyo, mkimbio wa kufunga mechi nane mtawalia wa mshambuliaji nyota wa Ureno anayechezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ulifikishwa kikomo.
Nahodha huyo wa Ureno aliondolewa uwanjani dakika ya 68 na nafasi yake akaingia kiungo wa Monaco Joao Moutinho.
Ronaldo alikuwa amefunga mabao 17 akichezea Real na mawili akichezea Ureno dhidi ya Misri Ijumaa katika kipindi hicho alichofunga mabao mechi nane mtawalia.

Kundi B

Ureno wamo Kundi B katika Kombe la Dunia pamoja na Uhispania, Morocco na Iran.
Lakini Uholanzi, ambao walishindwa 1-0 na England mechi ya kwanza Ronald Koeman akiwa mkufunzi wao, hawakufuzu kwa michuano hiyo itakayoanza mwezi Juni.

Messi kurejea dimbani

Kwingineko, Lionel Messi anapangiwa kurejea uwanjani kuwachezea Argentina mechi ya kirafiki dhidi ya Uhispania Jumanne.
Hakucheza mechi ambayo walilaza Italia 2-0 mjini Manchester Ijumaa kutokana na jeraha la misuli, lakini ameimarika na kuruhusiwa kuchezea taifa lake mjini Madrid.
Kocha wa Argentina Jorge Sampaoli amesema Messi alifanya mazoezi kama kawaida Jumatatu.

Argentina's Lionel Messi and Sergio AgueroHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLionel Messi amepona jeraha la misuli lakini mwenzake Sergio Aguero bado hawezi kucheza

Nyota huyo wa Argentina huenda akacheza dhidi ya wenzake wa Barcelona wanaochezea timu ya Uhispania Gerard Pique na Jordi Alba.
Uhispania walitoka sare 1-1 na Ujerumani mjini Dusseldorf Ijumaa, na kuendeleza mkimbio wao wa kutoshindwa chini ya Julen Lopetegui hadi mechi 17

Wednesday, 7 March 2018

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) adaiwa kutoweka Katika mazingira Ya Kutatanisha

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umesema mwenyekiti wake Mahmud Abdul Ormari Nondo hajulikani alipo na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha anapatikana akiwa salama kwa haraka.
Baba mdogo wa kiongozi huyo Mussa Mitumba akiwahutubia wanahabari pia ametoa wito kwa 'mwanawe' kurudishwa akiwa hai aendelee na kutafuta kutimiza ndoto zake.
Kiongozi huyo wa wanafunzi alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo, Tahliso.
Muungano huo unasema baada ya kuondoka afisi hizo, Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale.
"Ghafla katika hali ya kutatanisha, kuanzia saa 6 hadi saa 8 usiku alijitoa kwenye makundi yote ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp jambo lililozua taharuki miongoni mwa watu wengi na kuanza kutaka kujua nini kimemsibu," muungano huo umesema kupitia taarifa.
"Saa 9.09 usiku alituma ujumbe mfupi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP Paul Kisabo ujumbe uliosomeka 'Am at risk!' [Nimo hatarini]."
Muungano huo umesema juhudi za kuwasiliana naye kwa simu kufikia sasa bado hazijafanikiwa.
Wamesema wamepiga ripoti kwa jeshi la polisi katika kituo cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Taarifa ya chama hicho cha wanafunzi inasema Bw Nondo amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.
Wakati mmoja, anadaiwa kukamatwa na askari wa jeshi la polisi eneo la Milimani City na kutuhumiwa kwamba "analeta uchochezi wa baadhi ya wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu kuandamana."
"Mara kadhaa kumekwua na makundi ya watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimfuatilia na kumpa vitisho hivyo," taarifa hiyo inasema.
Muungano huo umesema viongozi mbalimbali wa TSNP wamekuwa wakipokea vitisho tofauti tofauti.

Sunday, 4 March 2018

Baraza la Maaskofu Lakomalia Katiba Mpya









Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limesema ili amani iendelee kuwepo majadiliano ndio nyenzo kuu itakayosaidia kuhuisha mchakato wa Katiba Mpya.

Pia limeitaka Serikali kuweka nia ya dhati na kutii kiu ya Watanzania iwapo wengi wao watahitaji mchakato wa Katiba Mpya uendelezwe.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa TEC, Padri Daniel Dulle, wakati akifungua kongamano la kujadili Katiba na ujenzi wa amani wakati wa uchaguzi lililoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichopungua mwezi mmoja kwa TEC kutoa kauli kama hiyo, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa Februari 11 mwaka huu, Baraza hilo katika ujumbe wake wa Kwaresma lilitoa msimamo katika masuala matatu kisiasa, kiuchumi na kijamii ambapo lilionya kutozingatia matakwa ya Katiba katika kuendeleza shughuli za kisiasa.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Padri Raymond Saba, Padri Dulle, alisema baada ya mchakato wa Katiba Mpya kukwama sasa ni fursa nzuri ya kuendeleza mchakato huo kwa njia ya majadiliano ili kudumisha amani.

“Majadiliano ni nyenzo ya kupambana na tabia ya ubinafsi, ili kujenga umoja huo lazima kuwepo na upendo, mshikamano na maridhiano ya watu na kila mtu kupewa nafasi ya kutoa maoni hata kama yanapingana na mtu mwingine na ukiwa unapatanisha kwa njia hiyo unaitwa mwana wa Mungu.

“Ndilo lengo la kukaa hapa na kujadiliana ili kujenga Taifa letu kwa lengo la kupata Katiba Mpya ambayo kila mmoja anaitamani. Kunapotokea mtafaruku ndipo kunakuwa na chuki kama kikundi kingine hakishirikishwi.  Haki na amani ni matunda tu, kwani ukosefu wa haki ni chanzo cha vita inayoacha makovu na chuki za kisiasa kwenye chaguzi. Kama tunataka kukwepa haya makovu lazima watu tujenge tabia ya kujadiliana,” alisema.

Alisema tangu miaka ya 1800, Kanisa Katoliki limekuwa likitoa miongozo kuhusu masuala ya utawala ili kudumisha amani.

“Suala la Katiba ni nia ya watu wote si ya mtu mmoja, ni sauti ya watu na kadiri watu wanavyohitaji sheria na miongozo. Pengine kikundi kikubwa kinahitaji kidogo hakihitaji cha msingi ni kuangalia wananchi wanahitaji nini kwani kwa mujibu wa ibara ya nane ya Katiba ya sasa, Katiba ni mali ya wananchi,” alisema.

Aidha, akichangia mjadala katika kongamano hilo, Profesa Mwesiga Baregu ambaye alikuwa akimwakilisha Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), James Mbatia, alionya Serikali kuhakikisha kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020, Katiba Mpya inapatikana.

Baregu ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema ni vema kukamilisha kiporo hicho cha Katiba kwa sababu viashiria vyote vya hatari vimekwishaonekana katika chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni hususani Jimbo la Kinondoni.

“Tujitahidi kwa vyovyote vile kuhakikisha uchaguzi unaokuja si tu wa haki lakini matokeo yake yawe ya kuaminika. Kwa sababu inaelekea chaguzi zetu kuwa ‘security election’.

“Uchaguzi uliopita Kinondoni tunaambiwa kuna vituo ambavyo polisi walizidi wapiga kura, huu uwapo wa polisi kwenye chaguzi ni tatizo kwa sababu inatafsirika kuwa lazima kutakuwa na machafuko au kuna kitu polisi wamegundua,” alisema.

Aidha, Profesa Baregu, alipendekeza njia tatu za kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa hali iliyopo lazima kuwepo na njia ya kuishawishi Serikali.

“Kwanza twende kwenye kura ya maoni, tunaweza kutangaza kura ya maoni kuhusu Katiba pendekezwa ila sijui kura ya maoni kama itaendeshwa kwa uhuru au haki. Kwa sababu hata katika Katiba pendekezwa tumeona asilimia 85 ya maoni ya wananchi yamenyofolewa.

“Pili kuundwe Bunge la Katiba lenye wajumbe wasiokuwa wabunge kwani hawa waliopo bungeni watatengeneza Katiba ya kuwalinda na tatu kuundwe tume ya wataalamu wa Katiba kama walivyofanya wenzetu Kenya, kwani mahali tulipofika lazima tutoke kwenye ujumla ujumla tuwe na mashinikizo ya kuitaka Serikali ifanye nini kabla ya uchaguzi mkuu ujao,” alisema.

Pamoja na mambo mengine also 

Monday, 26 February 2018

BREAKING NEWS: Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'sugu' Kahukumiwa Miezi Mitano Jela


BREAKING NEWS: Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'sugu' Kahukumiwa Miezi Mitano Jela




Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemuhukumu Miezi Mitano jela Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite ambapo amesema ameridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mteite amesema kuwa Mahakama imejikita katika sehemu kuu nne.

Amesema kuwa sehemu hizo ni kama washtakiwa walitamka Maneno ya fedheha, pia kama maneno waliyoyatoa yamebeba maudhui ya fedheha, pia kama maneno hayo yana mlenga Rais pamoja washtakiwa kama wana hatia ama lah.

Katika hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa moja Hakimu Mteite amesema amejiridhisha pasina kuacha shaka juu ya ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka.

Hakimu Mteite amesema Mahakama inakubaliana na hoja ya kwamba washtakiwa walitamka maneno ya fedheha dhidi ya Rais kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka ambao waliwasikia washtakiwa na kuwaona wakati wakitamka.

“Katika kesi hii mashahidi wengi ni askari, hivyo ni dhahiri wametoa maneno hayo,” -Hakimu Mteite

Pia kuhusu maneno hayo kumlenga Rais Magufuli, Hakimu Mteite amesema maneno hayo ya fedheha ni ya kitaifa, kwani masuala yanayogusa watu kuuawa ni ya kitaifa na ndio maana washtakiwa walitamka maneno (Rais Wetu).

“Tujiulize ni Rais yupi waliyemzungumzia ni wa Simba, Yanga ama Mbeya City hivyo Rais aliyezungumziwa hapa ni Magufuli kwani hakuna Magufuli mwingine anayetuongoza,”-Hakimu Mteite

Hakimu Mteite amesema kwa imani yake washtakiwa wana hatia.

“Kutokana na upande wa utetezi kuomba nafuu ya adhabu na upande wa mashtaka kutaka itolewe adhabu kali, nawahukumu miezi mitano jela,” -Hakimu Mteite.Ed

Saturday, 27 January 2018

Lowassa avaa gwanda kwa Mara ya Kwanza na kumnadi Mgombea wa CHADEMA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa leo  amepokewa kwa nderemo na wafuasi wa chama hicho.

Lowassa ambaye kwa mara ya kwanza leo Jumamosi Januari 27,2018 amevaa gwanda tangu ajiunge na Chadema mwaka 2015 aliwasili ofisi za chama hicho kanda ya Pwani zilizoko Magomeni, ambako yalianza maandamano kuelekea Mwananyamala ulikofanyika mkutano wa hadhara wa kampeni.

Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Ali Mapilau, Mwananyamala .

Akiongea katika mkutano huo, Lowassa amefunguka na kuwataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kuacha kumtaja taja mgombea Ubunge wa CCM Kinondoni Maulid Mtulia kwani mtu huyo ni wa hovyo hastaili kutajwa tajwa kwani kufanya hivyo ni kumpa kichwa.

"Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka kusema saizi tujiandae kulinda kura zetu" alisema Lowassa

Mbali na hilo Lowassa alimnadi Salum Mwalimu kwa kusema kuwa ni kijana safi ambaye anastahili kwenda Bungeni kuwasemea wananchi wa Kinondoni

Akizungumzia hatua ya Lowassa kuvaa Gwanda, Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Kinondoni, Rose Moshi amesema anadhihirisha kuwa ni kamanda na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi naye.

"Tulikuwa na hofu alipokwenda Ikulu, kuvaa kwake gwanda kunaonyesha kuwa ni mwenzetu," amesema.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Jerome Ulomi amesema Lowassa amedhihirisha kuwa ni mwana Chadem

Thursday, 7 December 2017

KISA CHA KUSISIMUA






Nakumbuka enzi hizo nikiwa mtoto mdogo nilikua na tabia ya kuchezea mawe kwa kuyarusha huku na huko.
Siku moja nilirusha jiwe likampata kuku wetu na kufariki palepale. Mama alikuwa akimhusudu sana yule kuku. Kwani alikuwa akitaga mayai mengi sana.
.
Wakati jiwe lilipompata yule kuku na kumuua palepale nilifikiri nilikuwa peke yangu katika mazingira yale. Kumbe dada yangu alikuwa upenuni mwa nyumba yetu akishuhudia jinsi nilivyomuua yule kuku.
.
Hivyo akaniambia, "Deo nimeona ulivyomuua kuku sasa nipe shilingi 50 vinginevyo nitamueleza mama kwamba ni wewe ndiye uliyemuua kuku wake."
.
Nikamwambia "Dada mi kwa sasa sina hiyo hela, tafadhali usimwambie mama, atanichapa kweli"
.
Siku iliyofuata, mama akamwambia dada yangu aoshe vyombo na kufagia uani, ila dada akamwambia mama: "Mama, Deo amesema atafanya usafi na kuosha vyombo yeye."
Halafu akaja kwangu na kuniambia: "Deo, osha vyombo na kufagia uani vinginevyo nitamwambia mama kwamba umemuua kuku wake". Bila kupinga nikaenda kuosha vyombo na kufagia.
.
Siku iliyofuata, mama alimwambia dada yangu aende kuteka maji kisimani na kujaza jaba. Akamwambia mama tena: "Mama, Deo amesema atachota na kujaza peke yake"
.
Hakafu akaja kwangu na kuniambua: "Deo, unamkumbuka yuke kuku uliyemuua? Jaza maji jaba ama sivyo nimueleze mama kwamba wewe ndiye uliyemuua kuku wake..." Hivyo nikajikongoja kuchota maji 'trip' za kutosha mpaka nikajaza jaba.
.
Siku hiyo hiyo jioni nikiwa nimechoka kweli, mama akamtuma dada aende sokoni kununua viazi na mahitaji mengine. Kwa mara nyingine tena akamwambia mama: "Deo amesema anahamu ya kwenda sokoni, anaomba aende yeye kununua."
.
Akaja kangu tena na kunuambia: "Deo, usisahau kuwa kuku bado amekufa, nenda sokoni na ununue viazi na mahitaji haya mengine, vinginevyo...."
Nilichoka!! Nilisimama na kwenda kwa mama huku machozi yakibubujika machoni mwangu, nikamkuta akiwa amekaa akisuka ukiri, nikamfuata na kupiga magoti mikono nimeifumba usawa wa kifua changu huku nikilia nikamwambia;
"Mama, nisamehe mimi. Mimi ndiye niliyemuua kuku wako ila haikuwa makusudi ni bahati mbaya tu katika kucheza kwangu, tafadhali sana mama nisamehe mimi."
.
Mama akanijibu huku akininyanyua: "Mwanangu ile siku umemuua kuku, nilikuwa dirishani nikiangalia kila kilichotokea. Dada yako alikufanya mtumwa wake kwa sababu hukutaka kuja kukiri kosa na kuomba masamaha."
"Lakini kwa kuwa umeona unateseka umekuja kukiri na kuomba msamaha, uko huru sasa, hatakutumikisha tena"

Maana ya yote hayo ni nini?
Kila mara tunavyotenda dhambi, Mungu anatuona na dhambi hizo zinatufanya tuwe watumwa. Kipindi ambacho tutakiri dhambi zetu na kutubu kwa muumba wetu basi atatuweka huru na tutaishi kwa amani, furaha na kheri.
Basi Mwenyezi Mungu atujalie tuwe na moyo wa toba ya kweli pale tunapokengeuka...Amen!
Comment na SHARE

Monday, 30 October 2017

BREAKING NEWS MBUNGE WA SINGIDA KASKAZINI RAZARO NYARANDU AJIUZURU NA KUOMBA KUHAMIA CHADEMA.













NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM


HISTORIA YAKE:

Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida.

Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987. Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 – 1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.

Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari, Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (Ukwata) 1991 – 1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro, Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.

Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.

Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo. Kiongozi huyu, sasa ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.

Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni, Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West, akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.

Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).

Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, China na nyinginezo. Pia, alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na k
I

Sunday, 17 September 2017

BREAKING NEWS *NACTE ; MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KATIKA VYUO VYA AFYA NA UALIMU VYA SERIKALI 2017/18


BREAKING NEWS *NACTE ; MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KATIKA VYUO VYA AFYA NA UALIMU VYA SERIKALI 2017/18* NACTE Imetangaza kumalizika kwa Uhakiki wa Udahili wa Wanafunzi wanaotarajia kujiunga kwenye vyuo vya Serikali, Afya na Ualimu , Unaweza kuangalia matokeo ya Selection kwa kubofya kwenye linki hapo👇👉👉http://www.tzjobconnection.com/2017/09/nacte-diploma-and-certificate-selection.html

*http://www.tzjobconnection.com/2017/09/nacte-diploma-and-certificate-selection.html

Friday, 15 September 2017

Tanzania yashangazwa na uchunguzi wa UN kuhusu Korea Kaskazini




Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Tanzania
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, waziri wa mambo ya nje Dkt. Augustine Mahiga, amesema licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mnamo mwaka 2014, Tanzania imepunguza kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.
"Hatuna ugomvi na Korea Kaskazini,lakini kitendo chao cha kutengeneza masilaha ya kuangamiza sio mazuri kwa heshima na usalama duniani.Ndiyo maana tukaanza kuchukua hizo hatua za kupunguza mahusiano." amesema Dr Mahiga kwa waandishi wa habari leo.
Waziri Mahiga ameongeza kusema kuwa, uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa.
Waziri huyo amesema anaelekea katika mkutano wa kawaida wa Umoja wa Mataifa, ambapo atatumia fursa hiyo kujibu tuhuma hizo kwa Baraza la Usalama.
Tanzania na Uganda ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazochunguzwa na Umoja wa Matiafa kwa tuhuma za kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Ripoti ya uchunguzi huo ilitolewa mnamo tarehe 9 mwezi wa Septemba. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linachunguza tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini inayogharimu dola za kimarekani milioni 12.5

MTANZANIA ALIYEFANIKIWA KUJIUNGA PSG MWAKA HUU


Saturday, 26 August 2017

Jeshi la Polisi Arusha lazuia mikutano ya Lema





Arusha. Jeshi la polisi mkoani Arusha, limepiga marufuku mikutano ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema iliyokuwa inaendelea katika jiji la Arusha ili kupisha maandalizi ya mtihani wa darasa la saba na mbio za Mwenge.
Katika barua ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, Mrakibu mwandamizi wa polisi (SSP),E.Tille ambayo imethibitisha na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,(SACP) Charles Mkumbo imeeleza kuwa, Lema amezuiwa kufanya mkutano kuanzia kesho Agosti 27 hadi Septembaa mosi.
"Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yeye ratiba kuanzia Agosti27 hadi Septema mosi kwa ajili ya kupisha maandalizi ya kuhitimisha mtihani wa darasa la saba na mwenge wa uhuru" ilisomeka barua hiyo na kushauri Lema kupanga mikutano kuanzia Septemba 8 mwaka huu.
Kamanda Mkumbo amesema, sababu kubwa ya kuzuiwa mikutano hiyo ni kwa kuwa wanahitajika polisi wa ulinzi na hivyo haiwezekani kupata polisi wa kulinda mikutano na pia kushiriki katika masuala ya mitihani na mwenge.
"Haya ni mambo ya kitaifa hivyo ndio sababu OCD amesitisha mikutano ya mbunge na mambo haya yakimalizika ataendelea na mikutano yake"alisema.
Akizungumza na mwananchi jana, Lema alisema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwani ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.
Lema amesema sheria ya bunge kifungu cha  nne fasihi ya  kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.
Lema amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama baada ya kubainika katika mikutano zaidi ya  10 ambayo amefanya katika jimbo la Arusha imekuwa na mafanikio makubwa na wananchi wa Arusha wamepata fursa ya kujua ukweli wa mambo mbali mbali.
"Hizi ni njama najua walipanga kuvuruga mikutano na kuharibu vyombo vyangu wakashindwa, wakanitakama kwa kuzidisha dakika 7 kwenye mkutano wangu mmoja nikawashinda kwa hoja sasa wameona wazuie kabisa na ikiwezekana watumie nguvu"alisema
Amesema sasa anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi ama aendelee na mikutano kwani kimsingi, maeneo ambayo mikutano imepangwa kufanyika sio ya shule .
"Sasa kesho Jumapili nipo nje ya mji eneo la Olmoti kuna maandalizi yapi ya mwenge na darasa la saba , ntakuwa na mkutano eneo la soko la Shuma kuna mkusanyiko kila siku wa watu, nitaathiri nini huo mwenge ambao utafika kuanzia Septemba 6"amesema
Hata hivyo amesema, baada ya barua hiyo na  kushauriana na mawaziri kadhaa na viongozi wa serikali, atalifikisha pia bungeni, kwani ni jambo la ajabu mbunge kuzuiwa kufanya mikutano kwasababu za mwenge na mitihani ya darasa la saba.
Amesema muda ambao umetakiwa na polisi afanye mikutano, anapaswa kuwa katika shughuli za kibunge jambo ambalo anaamini litaathiri ratiba za utendaji wa kazi zake.

MAN U VS LEICESTER CITY


Wednesday, 2 August 2017

FAITHFULLNES-KISA KIZURI CHA KUSISIMUA.



F A I T H F U L N E S S .
Alikuwa bafuni akioga...
"Honey, mama yako anakupigia..anataka umtumie pesa uliyomwambia mapema" Mkewe akawa akimwambia mumewe huku akiwa chumbani
"Sawa wife, naomba nisaidie ingia kwenye menu ya M-PESA kwenye simu yangu na mtumie shilingi laki moja" Mume akaongea kwa nguvu kutoka bafuni.
Mke akastaajabu. Inakuaje kirahisi rahisi hivyo Mumewe anamuamini na account yake ya MPESA.
"Baby, simu yako umeweka password. Mimi sijui password yako" mke akashauti tena kumwambia mumewe aliyepo bafuni...
"Password ya simu ni 2789. Na passowrd ya MPESA ni hiyo hiyo 2789" Mume nae akamjibu mkewe kutokea bafuni..
Akachukua simu ya mumewe, akaingiza password 2789 na simu ikawa unlocked. Akamtumia mama mkwe wake shilingi laki moja kama alivyoambiwa na mumewe.
Baada ya kutuma, akaingiwa na tamaa ya kupitia pitia sms kwenye simu ya mumewe. Akajiuliza maswali, kwanini mumewe aweke Password kwenye simu yake? Anaficha nini?
Akiwa anaangalia angalia chats mbalimbali facebook, WhatsApp na sms za kawaida kwenye simu ya mumewe hakuamini macho yake...
Chats nyingi zilionesha mumewe akimzungumzia yeye vizuri kwa marafiki zake na familia yake, aliona sms nyingine mumewe akimsifia hata mbele ya wanawake wengine...
Mke akatabasamu na kujawa na uso wa furaha baada ya kuona mumewe kwa kiasi gani anamjali. Akaona ni kwa kiasi gani mumewe yupo upande wake akimpigania..
Akaona baadhi ya wanawake waliokuwa wakimtumua sms za kiuchokozi chokozi jinsi walivyomwagwa, na baadhi yao aliona mumewe amewatumia picha yao ya pamoja na kuandika caption kwamba "Huyu ndiyo mwanamke nimpendae" Kitu ambacho kiliwaziba midomo wanawake wengine..
Kadiri alivyozidi kupekua simu ya mumewe ndivyo alivyozidi kugundua ni kwa namna gani mumewe ni rafiki mzuri kwa watu. Anao marafiki wengi kwenye chat list yake na marafiki wa kweli wakizungumza dili za maana..anapendwa na wengi na wanamkubali..
...Akaona ni kwa kiasi gani mumewe anawaombea watu, akiwaandikia sala na akiwabariki..akaona sms za kuwatia moyo wale waliokuwa wakimuandikia issue zozote za ushauri..
...Huyu mume wake ni wa ajabu, mume muaminifu, rafiki wa kweli, ndugu mwajibikaji kwa ndugu na wazazi wake, na mzungumzaji mzuri ambapo watu wengi wanapenda kuongea na kuchat nae..
..Mke akajisikia vibaya kwa hapo mwanzo kuwaza kwamba mumewe sio muaminifu jambo ambalo si kweli.
"Umeshamtumia mama pesa?" Mumewe akamuuliza huku akitoka bafuni akiwa amejifunga taulo.
"Ndio babylove..njoo hapa mpenzi wangu" Mke akamwambia mumewe huku akiinuka kitandani na kuweka simu pembeni.
Akamkumbatia mumewe kwa nguvu..
Akambusu kwa hisia kali. Uaminifu unampa raha mwanamke.
Akamvua taulo mumewe. Akamsukuma kitandani na kuanza kukanda kanda mwili wa mumewe..
"Oh baby, inaonesha una njaa na mimi eeh" Mume akaongea huku akisikilizia raha ya kupapaswa na mikono laini ya mkewe jambo lilofanya hisia zake ziamke.
Mke akakaa juu ya mumewe na wakafanya lile tendo lililoidhinishwa kwao...naam tendo la ndoa.
"Nakupenda sana swewtheart" mke akamwambia mumewe baada ya kumaliza mtanange.
"Nakupenda pia Darling". Mume akamjibu mkewe huku akimbusu kwenye paji la uso.
Siku chache baadae, alipomuuliza mumewe kwanini ameweka password kwenye simu yake, mumewe alimjibu kuwa ameweka password kwa sababu ya usalama wa nyaraka zake na pia kulinda usiri wa zile chats hot ambazo wamekuwa wakichat pamoja kama mke na mume. Kwamba watu wengine wasipate kuona maongezi yao.
Mke akakumbuka mambo ya kikubwa waliyokuwa wakichat na mumewe hasa pale anapokua mbali nae na akaona mantiki ya mumewe kuweka password kwenye simu yake.
______________________________
Usiwe mwepesi sana kumhisi mpenzi wako vibaya. Sio kila mtu ni msaliti kwenye ndoa yake. Kuna watu wako serious na mahusiano yao. Kwa sababu usaliti ni maamuzi ya mtu binafsi na wala sio bahati mbaya.
"Cheating is hard work. You gotta keep deleting text, keep locking your phone, keep deleting messages off of facebook, twitter, whatsap and think of lies..that's too much! rather be loyal"
Blessed .

Saturday, 29 July 2017

Korea Kaskazini yafanyia majaribio kombora jingine


Kombora lililorushwa na Korea Kaskazini
Image captionKombora lililorushwa na Korea Kaskazini
Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora, kulingana na maafisa wa Japan na Korea kusini.
Kombora hilo limeonekana likianguka katika bahari ya Japan kulingana na chombo cha habari cha kitaifa cha Japan.
Mapema mwezi Julai, Pyongyang ilidai kufanikiwa kulifanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza.
Kombora hilo ni la hivi karibuni katika msururu wa makombora yaliofanyiwa majaribio hatua inayokiuka marufuku ya UN.
Umbali wa kombora hilo haujulikani.
Umbali wake umepingwa lakini wataalam wanasema kuwa linaweza kufika Alaska nchini Marekani.
Msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema kuwa kombora hilo lilirushwa na kwamba habari zaidi zinasubiriwa.
Kombora hilo la hivi karibuni ni la 14 kurushwa na Korea Kaskazini 2017.
Kombora hilo lilirushwa kutoka mkoa wa Jagang kaskazini mwa taifa hilo , kulingana na chombo cha habari cha Korea kusini Yonhap.
Katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan Yoshihide Suga alisema kuwa kombora hilo lilisafiri kwa takriban dakika 45 ikilinganishwa na kombora la masafa marefu lililofanyiwa majaribio mapema mwezi Julai.
Anasema kuwa lilianguka katika bahari ya Japan, lakini sio katika maji ya himaya ya Japan.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameitisha mkutano wa kiusalama katikati ya usiku kulingana na Yonhap