Tuesday, 7 June 2016

CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuwakabili CHADEMA Waliojipanga 'Kumharibia' Rais Magufuli kwa Wananchi

SeeBait

Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi katika kipindi kifupi.

Alisema kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020. 

Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.

“Tunawaonya viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa kuwaeleza ukweli wananchi,”alisema Ole Sendeka.

Chadema wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu

Pele kupiga mnada medali zake zote


Mshirikishe mwenzako
Image copyrightACTION PLUS SPORTS IMAGES ALAMY STOCK PHOTO
Image captionPele kupiga mnada medali zake zote
Nyota wa soka kutoka Brazil, Pele, ameamua kupiga mnada medali zote alizoshinda na vitu vingine vyenye dhamani alivyopata wakati alipokuwa mchezaji nguli duniani .
Image copyrightDIVULGACAO I HALCYON GALLERY
Image captionMnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London
Mnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London na unatarajiwa kukusanya mamilioni ya pesa.
Image copyrightJULIENS
Image captionBaadhi ya medali za Pele zitakazouzwa leo mjini London
Wataalamu wanasema huenda mnada huo ukawa ndio mkubwa zaidi wa vifaa vya michezo kuwahi kufanyika.
Image captionMedali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa
Medali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa wakati wa mnada huo.
Image copyrightJULIENS
Image captionViatu alivyochezea katika kombe la dunia
Nyota huyo wa zamani amesema atatoa sehemu ya fedha zitakazo patikana kwa mashirika ya kutoa misaada na kuongeza kwamba angelipenda historia yake kufurahiwa na kuonyesha katika makaazi ya watu na makavazi kote duniani.
Image copyrightGETTY
Image captionPele ambaye alianza kuchezea Brazil mika 60 iliyopita anasalia kuwa mfungaji bora zaidi wa mabao nchini humo.
Pele ambaye alianza kuchezea Brazil mika 60 iliyopita anasalia kuwa mfungaji bora zaidi wa mabao nchini humo

Thursday, 26 May 2016

Klabu ya soka yafungwa mabao 44 Ecuador

Mshirikishe mwenzako
Pelileo Sporting ClubImage copyrightSUPPLIED
Image captionUwanja ulikuwa na mashabiki 200 wakati wa mechi hiyo
Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.
Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina alifunga mabao 18.
Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.
Mwandishi wa habari Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.
Anasema ligi ya daraja la tatu ya Ecuador huwa na ushindani mkubwa.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36-0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopita.
Mwenyekiti wa Arbroath FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka 1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.
44-1
matokeo ya mechi kati ya Pelileo Sporting Club na Indi Native nchini Ecuador
  • 18 mabao aliyofunga mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina
  • 131 miaka ambayo rekodi ya sasa, Arbroath 36-0 Bon Accord, imedumu
Bw Christison ameambia BBC Scotland: "Ni rekodi ambayo tumeishikilia kwa miaka 130.
"Tutasikitika sana kama klabu iwapo tutaipoteza rekodi hii ambayo kama jiji twajivunia sana.
“Ilifahamika sana kwamba wakati huo kipa wetu hata hakugusa mpira na alisimama kwenye goli na mwavuli kwani mvua kubwa ilikuwa inanyesha.
"Lakini tutasubiri uamuzi wa maafisa wa Guinness.”
Siku hiyo ya ushindi wa Arbroath mwaka 1885, Dundee Harp walilaza Aberdeen Rovers 35-0.
Ingawa mwamuzi alisema mabao yalikuwa 37, karibu wa Dundee Harp alisema alirekodi 35 pekee, mabao ambayo mwishowe yalitambuliwa.
Mwaka 2002, mechi ya ligi kuu ya Madagascar ilitoa matokeo ya kushangaza baada ya mabingwa wateule AS Adema kulaza mahasimu wao wa jadi Stade Olympique I'Emyrne 149-0. Wachezaji wa Olympique walijifunga makusudi kwa hasira kulalamikia uamuzi wa refa.
Matokeo ya mechi hiyo hayakutambuliwa kimataifa.

Maandamano ya kumpinga Kabila yafanyika DRC




Mshirikishe mwenzaMaandamano ya upinzani yanafanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph kabila atasalia madarakani baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi hautafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Maandamano hayo yamepigwa marufuku katika maeneo mengine ikiwemo mji wa Lubumbashi nyumbani kwa mgombea wa urais wa Upinzani Moise Katumbi.
Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.
Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.


Image caption
Mjini Goma katika eneo la Birere,amesema kuwa ni mchezo wa paka na panya ambapo vijana wamekuwa wakijibizana na polisi kwa kuwarushia mawe huku nao maafisa hao wakiwatupia vitoa machozi.
Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa polisi.

Monday, 23 May 2016

Simba wakamatwa na kufungiwa kwa kuwaua watu India



Mshirikishe mwenzako
Image copyright
Image captionSimba
Maafisa wa misitu nchini India wamewakamata na kuwafungia simba 13 wa bara Asia, magharibi mwa India baada ya watu watatu kuuawa.
Simba hao walizungukwa na kukamatwa baada ya kijana mmoja kutolewa katika kijiji chake, kuuawa na kuliwa kiasi.
Watu wengine wawili waliuawa katika kipindi cha miezi miwili ijapokuwa maafisa wanasema kuwa mashambulio kama hayo huwa nadra.
Simba hao wa Asia wanaoorodheshwa kuwa hatari ni miongoni mwa simba 500 wanaoishi katika msitu wa Gir mjini Gujarat.
Afisa mkuu wa uhifadhi wa wanyama pori katika mji huo J A Khan,alisema simba hao walikamatwa katika eneo moja la mashariki mwa eneo hilo la uhifadhi wa wanyama pori.
''Simba ambao wanawawinda binaadamu watakamatwa na kuchunguzwa huku waliosalia wakirudishwa msituni'',alisema bw Khan

Manchester United yamfuta kazi Louis van Gaal

Mshirikishe mwenzako
Image copyrightEPA
Image captionLouis Van Gaal
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United, huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.
Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.
Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.
Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.

MTU AFARIKI KATIKA MAANDAMANO KENYA 




Image caption
Mwanamume mmoja amefariki wakati wa maandamano ya upinzani katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, watu walioshuhudia wameambia BBC.
Mwanamume huyo anadaiwa kufariki wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji hao wanaowashinikiza maafisa wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) kujiuzulu.
Hospitali moja mjini humo imethibitisha kwamba mwili wa mwanamume umefikishwa katika hospitali hiyo lakini chanzo cha kifo chake hakijathibitishwa.
Jijini Nairobi, maafisa wa polisi wametawanya waandamanaji waliokuwa wakitaka kufika katika afisi kuu za tume hiyo.
Shughuli za kibiashara katika jiji hilo zimetatizika pakubwa.
Polisi wamekuwa wakikabiliana na makundi ya wafuasi wa muungano huo wa upinzani wa Cord kwa mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.
Maandamano pia yameshuhudiwa katika miji mingine kama vile Mombasa na Kakamega.
Viongozi wa CORD wanasema mmoja wa maseneta wa muungano huo amekamatwa wakati wa maandamano ya leo mjini Kakamega, magharibi mwa Kenya.
Miji

Leo imekuwa wiki ya nne ya maandamano hayo ya upinzani.
Wiki iliyopita, polisi walikabili vikali waandamanaji na baadaye walishutumiwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kwa kutumia "nguvu kupita kiasi”.
Rais Uhuru Kenyatta wiki jana alisema upinzani unafaa kutumia utaratibu uliowekwa kikatiba iwapo unataka kufanikisha mabadiliko katika tume ya uchaguzi.
Ametoa wito kwa “upinzani kuonesha siasa komavu badala ya kutumia njia haramu kuvutia hisia.”