Monday, 20 June 2016

Bajeti Kuu Ya Serikali 2016/2017 Yapitishwa Bungeni Kwa Asilimia 100.......Serikali Yasema Kodi ya Kiinua Mgongo Itakatwa kwa Watumishi Wote Akiwemo Rais


Serikali ya Tanzania imepitisha bajeti ya shilingi trilion 29.5 kwa kupigiwa kura huku wabunge wa upinzani wakiwa wametoka nje wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na plasta ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhika na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakigomea vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika huyo

Katika vikao vya Bunge la 11, wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa wakisusia vikao hivyo kwa takribani siku 23 sasa kwa madai ya kutokubaliana na ukandamizaji unaofanywa na Naibu Spika wa Bunge Dkt.Ackson Tulia.

Wakichangia bajeti hiyo, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage wamesema bajeti hiyo inalenga kukuza uzalishaji.

Akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Bajeti hiyo ikiwa ni pamoja na ya kuongeza fedha katika ofisi ya mkaguzi wa serikali CAG ili kutanua wigo wa ukaguzi pamoja na kuachana na mpango wa kuanza kuwakata kodi wabunge katika mafao ya kiinua mgongo ya Wabunge, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema msimamo wa serikali upo pale pale.

Kuhusiana na makato ya kodi kwenye mafao ya wabunge, Dkt Mpango amesema kuwa serikali imeamua kuwa itakata kodi hiyo kwa viongozi wote wa kisiasa wakiwemo wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais pia, ili kuweka usawa katika makato ya kodi nchini.

Baadaye jioni wabunge walipiga kura mmoja mmoja kupitisha bajeti hiyo, ambapo wabunge wote 251 waliokuwemo bungeni walipitisha bajeti hiyo kwa kauli moja, ambapo kila mbunge alijibu "Ndiyo" akimaanisha anaipitisha bajeti hiyo.

Mapema Asubuhi mara baada ya dua, wabunge wa upinzani waliziba midomo yao kwa karatasi na Plasta na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhika na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.

Mbunge wa Vunjo Kupitia chama cha NCCR Mageuzi, Mhe. James Mbatia kwa niaba ya wabunge hao alisema hawataacha kulalamikia ukiukwaji wa sheria unaofanywa na kiti cha Naibu Spika.

Monday, 13 June 2016

 Alichokisema Zitto Kabwe baada ya kutoka mafichoni 

SeeBait
Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya huku akilaani mbinu za Jeshi la Polisi kutaka kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu unaotakiwa.

Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti Zitto kutofahamika alikokuwa baada ya simu zake zote kutopatikana huku viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa na polisi baada ya kubaini njia za uviziaji wa kumkamata nyumbani
kwake.

"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu wakiwa na magari matatu ila hawakufanikiwa, siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa tayari kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo kuviziana, kama nina makosa kwa nini wanivizie," amesema Zitto Kabwe na kuongeza;

''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari
 

''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa
 

''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia
 

''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli .Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie
 

''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta
 

''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG. Kwa hali Hii anayokwenda Magufuli ajiandae kuwa rais wa term moja kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa .
 

''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti
 

''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''
 

''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao
 

''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa
 

''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

Wakili aliyepigwa na kupasuliwa nguo mbele ya majaji China

Mshirikishe mwenzako
Image captionWakili wa China aliyevuliwa nguo
Mawakili wengi wa China wamenyanyaswa,kukamatwa na hata kufungwa jela lakini picha ya mmoja wao aliyekuwa na nguo zake zilizovuliwa na maafisa wa polisi imevutia hisia nyingi nchini China.
Wu Liangshu alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Qingxiu akiwa amevalia koti lake na suruali ya ndani ikionekana.
Yeye na mawakili wengine waliambia maafisa wa mahakama kwamba alishambuliwa na maafisa watatu katika mahakama moja mbele ya majai mawili ambao walikataa ombi lake la kutaka kuanzisha kesi katika mahakama ya wilaya ya Nanning Mkoani Guangxi.
Bw Wu alipewa nguo nyengine lakini alijua uwezo wa kile alichokuwa akipanga kukifanya.''Asante alisema''.
Wakili huyo baadaye alitembea kupitia mlango wa mbele akiwa amebeba nakala zake za mahakamani akiwa na kalamu iliowekwa katika mfuko wa shati liliposuliwa.
Baadaye alipigwa picha nje ya jengo hilo la mahakama

Polisi wabaini maandalizi ya shambulizi,Marekani

Mshirikishe mwenzako
Image copyrightEPA
Image captionMashambulizi ya Orlando Marekani
Wakati wakazi wa Orlando na Marekani kwa ujumla wakiomboleza kuuawa kwa watu 50 kwa kupigwa risasi na watu wanaodhani kwa walikuwa katika hafla ya watu wenye kushiriki mapenzi ya jinsia moja mtu mmoja amekamatwa na silaha Los Angles Marekani.
Awali taarifa za kiintelijensia zinasema kuwa mtu huyo aliyekamatwa kuhudhuria hafla moja ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja huko Los Angeles Marekani.
Polisi wanasema wanamzuilia mtu huyo James Howell kutoka Indiana kwa kupatikana na silaha nzito zikiwemo bunduki tatu aina ya assault rifles, kemikali na kizuia gesi cha kuvaa usoni

Eritrea na Ethiopia zapigania eneo la mpakani

Mshirikishe mwenzako
Image captionEritrea na Ethiopia zapigania eneo la mpakani
Eritrea imeishtumu Ethiopia kwa kutekeleza shambulio katika mpaka wake ambao una ulinzi mkali.
Wakazi katika eneo la Tsorona wanasema wamesikia milio ya risasi na kuona wanajeshi wakielekea katika mpaka.
Hata hivyo Waziri wa habari wa Ethiopia amesema hafahamu lolote kuhusu vita hivyo.
Zaidi ya watu laki moja walifariki katika mapigano yaliyodumu mika miwili na nusu katika ya mataifa yote mawili.
Kamati ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa eneo linalozozania linapaswa kuwa la Eritrea, lakini Ethiopa haijawahi kukubali uamuzi huo.
Mwandishi wetu Emmanuel Igunza anasema kuwa wakaazi wa eneo la Tsorona kwenye mpaka wa Ethiopia na Eritrea wanasema kuwa wamesikia milio mikubwa ya risasi kuanzia Jumapili asubuhi.
Pia wameripoti kuwaona wanajeshi wa Ethiopia waliojihami kwa silaha kali wakipita katika mji huo wakielekea maeneo ya mpakani.
Lakini waziri wa habari wa Ethiopia ameiambia BBC kuwa hafahamu lolote kuhusu mapigano hayo.
Eritrea kwa upande wake imetoa taarifa inayoshtumu Ethiopia kwa kuanzisha mapigano hayo.
Image captionEritrea imeishtumu Ethiopia kwa kutekeleza shambulio katika mpaka wake ambao una ulinzi mkali.
Nchi hizo mbili zimekuwa na mzozo wa miaka mingi kuhusu eneo la Badme ambalo kamati iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilisema inapaswa kuwa ya Eritrea.
Lakini Ethiopia imepinga uamuzi huo ambao hadi kufikia sasa haujatekelezwa kikamilifu.
Zaidi ya watu elfu mia moja walifariki kati ya mwaka wa 1998 na mwaka wa 2000 katika mapigano makali kuhusu mpaka.
Mapigano katika eneo hilo la mpakani yamefanyika awali lakini ni nadra sana.

Tuesday, 7 June 2016

CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuwakabili CHADEMA Waliojipanga 'Kumharibia' Rais Magufuli kwa Wananchi

SeeBait

Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi katika kipindi kifupi.

Alisema kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020. 

Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.

“Tunawaonya viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa kuwaeleza ukweli wananchi,”alisema Ole Sendeka.

Chadema wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu

Pele kupiga mnada medali zake zote


Mshirikishe mwenzako
Image copyrightACTION PLUS SPORTS IMAGES ALAMY STOCK PHOTO
Image captionPele kupiga mnada medali zake zote
Nyota wa soka kutoka Brazil, Pele, ameamua kupiga mnada medali zote alizoshinda na vitu vingine vyenye dhamani alivyopata wakati alipokuwa mchezaji nguli duniani .
Image copyrightDIVULGACAO I HALCYON GALLERY
Image captionMnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London
Mnada huo utakaodumu muda wa siku tatu, unaanza leo mjini London na unatarajiwa kukusanya mamilioni ya pesa.
Image copyrightJULIENS
Image captionBaadhi ya medali za Pele zitakazouzwa leo mjini London
Wataalamu wanasema huenda mnada huo ukawa ndio mkubwa zaidi wa vifaa vya michezo kuwahi kufanyika.
Image captionMedali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa
Medali zote alizoshinda wakati wa kombe la dunia pia zitauzwa wakati wa mnada huo.
Image copyrightJULIENS
Image captionViatu alivyochezea katika kombe la dunia
Nyota huyo wa zamani amesema atatoa sehemu ya fedha zitakazo patikana kwa mashirika ya kutoa misaada na kuongeza kwamba angelipenda historia yake kufurahiwa na kuonyesha katika makaazi ya watu na makavazi kote duniani.
Image copyrightGETTY
Image captionPele ambaye alianza kuchezea Brazil mika 60 iliyopita anasalia kuwa mfungaji bora zaidi wa mabao nchini humo.
Pele ambaye alianza kuchezea Brazil mika 60 iliyopita anasalia kuwa mfungaji bora zaidi wa mabao nchini humo