Saturday, 5 November 2016

Trump aimarika huku Clinton akiendelea na kampeni




Kura ya maoni inaonyesha kuwa kura yoyote itakayopigwa itatekeleza wajibu muhimu kuamua ni nani ataongoza.Image copyrightAP
Image captionKura ya maoni inaonyesha kuwa kura yoyote itakayopigwa itatekeleza wajibu muhimu kuamua ni nani ataongoza.

Huku kura ya maoni ikionyesha kuwa Donald Trump anaendelea kupata uungwaji mkono, Hillary Clinton naye amekuwa akifanya mikutano katika majimbo ambayo yameonekana kuwa ngome ya chama cha Democratic.
Kwa sasa pande zote zinafanya mikakati ya kuwashauri wapigaji kura kupiga kura baada ya kuwarai wale ambao bado hawajafanya uamuzia.
Inadhaniwa kuwa zaidi ya watu milioni 37 tayari wamepiga kura.
Huku ikiwa zimebakia siku tatu pekee kabla ya upigaji kura mawakili wa chama cha Democratic wameanza kuwasilisha kesi mahakamani wakisema maajenti wa Donald Trump wameanza mtindo wa kuhakikisha kuwa watu fulani hawapigi kura siku ya upigaji kura.
Bwana Trump ametoa wito kwa mawakili wake watekeleze wajibu wa wachunguzi ili kujiepusha na ulaghai na hali ambapo mtu haibi kura.

Bi Clinton aliungana na Jay Z na mkewe Beyonce katika jimbo la OhioImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionBi Clinton aliungana na Jay Z na mkewe Beyonce katika jimbo la Ohio

Katika jimbo la Ohio, Jaji ametoa amri dhidi ya kundi la kampeni la Donald Trump lihakikishe kuwa halishiriki katika kuwatisha watu wanaotaka kupiga kura.
Wakati huohuo Bi Clinton ameungana na mwanamziki wa mtindo wa Rap, Jay Zee katika hafula maalumu inayokusudia kuwarai wapiga kura wenye asili ya Afrika wajitokeze kwa wingi Jumanne kupiga kura.
Kura ya maoni ya sasa inaonyesha kuwa kura yoyote itakayopigwa itatekeleza wajibu muhimu kuamua ni nani atakayeongoza.
Inaonekana kuwa Donald Trump amekaribiana sana na Bi Clinton na hakuna uhakika kuwa ni nani atakayeshindwa kwa wakati huu.

Bodi ya Mikopo Elimu Ya Elimu ya Juu Yaagizwa Kuwapa Wanafunzi Fedha Zao ifikapo Leo


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB), imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo zinapelekwa vyuoni ifikapo leo. 

Agizo hilo lilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wabunge mbalimbali kuomba miongozo kwa Spika kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17. 

Mwongozo kwa Spika ulitiliwa mkazo na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete aliyeeleza kuwapo taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa wanafunzi wanataka kugoma kwa kukosa fedha za mikopo. 

Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga aliitaka Serikali kutoa maelezo. 

Akitoa kauli ya Serikali, Profesa Ndalichako alisema fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki moja iliyopita. 

“Tatizo lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au la lakini hawakujaza fomu. Serikali haitatoa mkopo kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu. Na waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”alisema. 

Kuhusu wanaoendelea na masomo, Profesa Ndalichako alisema wanafunzi wote wanufaika na wanaoendelea na masomo wataendelea kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa mwaka uliopita. 

Alisema wanafunzi ambao vyuo vyao vimewasilisha HELSB taarifa za matokeo, Bodi imekwishawatumia fedha vyuoni kwa ajili ya kuwapa mikopo wanafunzi hao. 

Hata hivyo, alisema taratibu za kuwabaini wanafunzi wenye sifa zinaendelea na wasio na sifa wataendelea kuondolewa kupata mikopo. 

Pia, alikiri kuwa ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo umeathiri kasi ya kutuma fedha vyuoni. 

“Wizara yangu imekwishaagiza vyuo vyote ambavyo havijawasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi wao kwa mwaka wa masomo uliopita, kufanya hivyo mara moja,”alisema. 

Ndalichako alisema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Sh71.042 bilioni zilikwishatumwa vyuoni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.

Akizungumzia utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17, Ndalichako alisema katika mwaka huo, Sh483 bilioni zimetengwa na zimelenga kutoa mikopo kwa wanafunzi 119,012, wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo na wa mwaka wa kwanza 25,717.

Ndalichako alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 wanafunzi 58,010 walidahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na orodha yao iliwasilishwa HELSB na hadi Novemba 2, mwaka huu, wanafunzi 21,190 wa mwaka wa kwanza wamepewa fedha. Kati yao 4,321 ni yatima, 118 wenye ulemavu na 87 ni waliosoma sekondari kwa ufadhili wa taasisi mbalimbali.

Sunday, 9 October 2016

Viongozi wa Republican wazidi "kumtema" Donald Trump


o
Viongozi wakuu wa chama cha Republican wanazidi kuondoa uungaji wao mkono kwa Donald Trump kwa matamshi yake ya kuwadhalilisha wanawake.
Seneta John McCain
Image captionSeneta John McCain
Miongoni mwa wanasiasa wa hivi punde zaidi ni pamoja na aliyekuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, na aliyegombea kiti cha urais nchini humo, Senator John McCain.
Lakini Trump amesema kwamba hatajiondoa kutoka katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti hicho licha ya malalamishi kutoka kote duniani kutokana na matamshi yake ya kuudhi kuwahusu wanawake, aliyo-yatoa mwaka 2005.
Zaidi ya wanasiasa 24 wa chama chake cha Republican, sasa wamesema hadharani kuwa hawamuungi mkono bilionea huyo na wanamtaka kumuachia mgombea mwenza Mike Pence nafasi ya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa Marekani hapo mwezi Ujao.
Miongoni mwa wanaolaani matamshi hayo ya Trump ni pamoja na mkewe Trump- Melania.
Aliyekuwa waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice
Image captionAliyekuwa waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice
Amesema kuwa licha ya kuendelea kumuunga, analaani matamshi hayo mapotovu dhidi ya wanawake.
Spika wa Bunge Paul Ryan, alizomewa na kushangiliwa kwa wakati mmoja, katika mkutano mmoja wa kisaiasa baada ya kukataa kutumia jukwaa moja na Bwana Trump.

Tuesday, 4 October 2016

BODI YA UDHAMINI HAIMTABUI LIPUMBA



By Wandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Mazingira yanaweza kuwa tofauti, lakini mgogoro unaoonekana kukiandama Chama cha Wananchi (CUF) unaanza kuchukua sura iliyodhoofisha vyama vingine vya upinzani vilivyokuwa na nguvu baada ya kurejeshwa kwa siasa za ushindani.
CUF inapitia kwenye kipindi kigumu kutokana na vyombo vyake vya juu kutofautiana na Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ameghairi uamuzi wake wa kujiuzulu, takriban mwaka mmoja baada ya kukiacha chama hicho katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Wakati Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad anaungana na zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa vikao vyote vya juu, Profesa Lipumba anaungwa mkono na wajumbe wachache wa mkutano mkuu na kikundi cha wafuasi wake cha jijini Dar es Salaam.
Profesa Lipumba na wafuasi wake wamepata nguvu zaidi baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kueleza msimamo wake kuwa anamtambua msomi huyo kuwa ndiye mwenyekiti halali wa CUF, uamuzi uliowafanya waende hadi ofisi kuu za chama na kujimilikisha hadi leo.
Hali hiyo ndiyo iliyowahi kuikumba NCCR-Mageuzi iliyokuwa na nguvu kubwa baada ya nchi kurejea kwenye siasa za ushindani, lakini mgogoro mkubwa wa uongozi ulisababisha kipoteze nguvu zake.







Wakazi wa Dar kupata huduma ya bure ya Wi-Fi



Mshirikishe mwenzako
Mji Wa Dar es SalaamImage copyrightAFP
Image captionMpango wa kutoa huduma ya Wi-Fi ni sehemu ya mpango mkubwa wa awamu tano wa kustawisha miji
Makamu wa rais nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza mpango wa kuzindua mradi ambao utapelekea kuwekwa kwa huduma ya mtandao wa Wi-Fi katika maeneo ya umma na yale ya burudani mjini Dar es Salaam.
Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo basi kuimarisha uchumi.
''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu wataweza kupata huduma ya mtandao," alisema kupitia taarifa, kwa mujibu wa gazeti la serikali ya Daily News.
Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.
Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City' nchini Tanzania.

Saturday, 17 September 2016

Mamba mkubwa Big Daddy kufanyishwa ndoa Mombasa



Mamba
Image captionMamba aliyepewa jina Big Daddy (kulia) na wenzake

Mmoja ya mamba wakubwa zaidi duniani kwa jina Big Daddy, ambaye anafugwa katika katika Mamba Village, mjini Mombasa, atafungishwa ndoa rasmi na wake zake wawili, Salma na Sasha.
Hafla hiyo ya kipekee inatarajiwa kufanyika Aprili tarehe 29 mwakani mjini Mombasa.
Mamba huyo ana uzani wa tani moja na anaaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100.

Big Daddy
Image captionBig Daddy alianza kuishi Mamba Village mwaka 1986

Waandalizi wa ndoa hiyo wanasema wameamua kumsaidia Big Daddy afanye harusi baada ya kuwapa wake zake wawili penzi motomoto kwa miaka 30.
Alikuwa amewekewa mamba wengine wawili aishi nao lakini akawala.
David Mbatu, mmoja wa wahudumuwa Mamba Village wanaosaidia kuandaa harusi hiyo anasema keki ya harusi itakuwa ni mfupa wenye mnofu wa nyama na damu.
"Big Daddy alikuja hapa mwaka 1986 tukamchagulia wake wanne, akaua wake wawili akabaki na hawa wawili. Sasa amekuwa na hao wawili kwa miaka 30. Sasa kama ameonyesha upendo wa miaka hiyo basi tuonyeshe mfano pia mamba anaweza akafanyiwa ndoa," anasema.

Mamba Village
Image captionMamba Village

Mipango ya awali ilikuwa harusi ifanyike mwezi Desemba lakini baadaye wakakumbuka kwamba kipindi hicho mamba huwa wana mayai.
"Hajajua. Atajua tu siku hiyo, kwa sababu tutafanya mazoezi kumuonyesha kwamba kuna kitu fulani kitakuja. Wajua mamba ana kumbukumbu nzuri sana."
Kwa vile hawawezi kuwavalisha mamba hao nguo za harusi, watajaribu kuwapamba.
Maimuna Siraj pia ni miongoni mwa wanaopanga harusi hiyo.
"Ukiangalia mapenzi yao yanavutia, mara wenyewe wanakumbatiana, wanapigana busu. Na ukiangalia ni sehemu moja. Kama ni mtu mwingine, angetengea nyumba mbalimbali au boma kando kando."

Big Daddy
Image captionMaimuna anasema zamani Big Daddy alikuwa na ukali kupita kiasi

"Kabla apate hawa mamba, alikuwa anawala mamba wengine. Lakini hawa wanawake wameweza kumtuliza."
Sasha alitoka bara lakini Salma asili yake ni pwani.

Mamba wengi watakuwa wamebeba mayai mwezi Desemba
Image captionMamba wengi watakuwa wamebeba mayai mwezi Desemba

Paul Mutua, meneja wa bidhaa wa Mamba Village, watalii na wageni mashuhuri wanatarajiwa kufika kushuhudia harusi hiyo.
Anasema wanapanga kumwalika waziri wa utalii Najib Balala na hata Rais Uhuru Kenyatta.
"Tutakuwa na watalii kutoka humu nchini na tunatarajiwa wageni hata kutoka nje ya nchi," anasema.

Saturday, 3 September 2016

VITUKO VYA MUGABE


Rais Robert Mugabe atoa mzaha kuhusu afya yake



Robert MugabeImage copyrightREUTERS
Image captionRais Mugabe amesema alikuwa Dubai kwa masuala ya kifamilia

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepuuzilia mbali taarifa za hivi karibu za uvumi juu ya afya yake, kwa kutoa mzaha kwamba alikufa na akafufuka.
Akionekana mwenye furaha, Mugabe mwenye umri wa 92, aliyasema hayo alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare akitokea nje ya nchi.
Taarifa ya safari yake ilisema kuwa ndege yake ilikuwa ikielekea mashariki mwa Asia, na kwamba badala yake ilikwenda Dubai.
Bw Mugabe alisema kuwa alikwenda huko kwa masuala ya kifamilia.
Mnamo mwezi Mei, Mke wa Mugabe, Grace, alisema kuwa mumewe ataongoza nchi hata akiwa kaburini.
Taarifa za uvumi kuhusu safari zake za ndege na nyinginezo, zilisababisha kuenea kwa tetesi kwamba afya ya Bw Mugabe ilikuwa mbaya na kwamba alikwenda Dubai kwa matibabu ama hata alikuwa tayari amepoteza maisha.
Tovuti ya Gazeti linalochapishwa kila siku la Southern Daily, ilituma makala yenye kichwa cha habari "Robert Mugabe anauwa kiharusi, Mnangagwa sasa ndie rais wa mpito wa Zimbabwe".
Emmerson Mnangagwa ni makamu rais wa Zimbabwe