Wednesday, 7 December 2016

Tanzania: Uhusiano wetu na Malawi ni shwari



Ramani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake.Image copyrightTZAFFAIRS.ORG
Image captionRamani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake.
Serikali ya Tanzania imesema mzozo kuhusu mpaka wake na Malawi katika Ziwa Malawi kwa sasa unashughulikiwa na jopo la maais wastaafu, na kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeimarika.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia taarifa, imesema kwamba licha ya kuwepo kwa mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, uhusiano wa nchi hizo mbili ni mzuri.
"Ukweli ni kuwa, mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwa sasa upo chini ya Jopo la Viongozi Wastaafu wa Afrika wanaotokea kwenye nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)," taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema.
"Jopo hilo linaongozwa na Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini."
Taarifa hiyo ya serikali imetolewa baada ya wasiwasi kutanda kuhusu uwezekano wa kuzuka tena kwa mzozo kati ya nchi hizo kutokana na ramani iliyodaiwa kutolewa na Tanzania ikionyesha kuwa inaamiliki nusu ya Ziwa Malawi au Nyasa.
Ramani hiyo ya Tanzania ilionyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake, lakini Malawi nayo inadai kuwa eneo hilo lote ni lake.
Malawi ilikuwa imewasilisha ombi kwa Umoja wa Mataifa, Mungano wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa kuingilia kati.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Malawi, Rejoice Shumba aliambia gazeti la The Nation la Malawi kuwa nchi yake ilikuwa imeandika barua kwa mashirika makuu duniani ikiyataka kupuuzilia mbali ramani ya Tanzania.
Serikali ya Tanzania hata hivyo imesema kwamba jopo hilo ambalo liliundwa na Umoja wa Afrika kupitia Jukwaa la Viongozi Wastaafu wa Afrika kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro huu, linaendelea na kazi hiyo kwa kupitia taarifa mbalimbali na maandiko yaliyowasilishwa kwao na Tanzania na Malawi.
Vile vile, jopo lilikwisha zikutanisha pande zote mbili katika mashauriano ya awali yaliyofanyika nchini Msumbiji.
"Wizara inapenda kuujulisha umma kuwa licha ya kuwepo kwa mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, mahusiano ya nchi hizi mbili yamezidi kuimarika siku hadi siku katika Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii," taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilisema.
"Hata wananchi wa pande zote mbili za Ziwa wameendelea kuishi kwa amani na ushirikiano wa karibu."
Kwa mujibu wa Tanzania, nchi hizo mbili zinatarajia kuwa na mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano mapema mwakani ambao utawaleta watalaam wa nchi hizo mbili kutoka sekta mbalimbali.
Msukosuko uliibuka mwaka 2011 wakati Malawi ilianza shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo.Image copyrightAFP
Image captionMsukosuko uliibuka mwaka 2011 wakati Malawi ilianza shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo.
Lengo la mkutano huo litakuwa kujadili changamoto za ushirikiano katika sekta hizo, kubaini maeneo mapya ya ushirikiano pamoja na kuweka mikakati ya kutekeleza miradi ya pamoja itakayokubaliwa baina ya pande hizi mbili.
Aidha, watakaohudhuria watajadili masuala ya ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, fedha, nishati, utalii, ulinzi na usalama uhamiaji, uvuvi na ardhi.

Nini hasa kinazozaniwa?

Fahari ya nchi na maswala ya kujiendeleza kiuchumi kwa Malawi na Tanzania kila mmoja akisimama kidete kusisitiza msimamo wake.
Kwa Tanzania, ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago Niassa.
Malawi na Tanzania ni koloni za zamani za Uingereza wakati Msumbiji ilikuwa chini ya ukoloni wa Ureno. Uingereza iliichukua Tanzania kutoka kwa Wajerumani baada ya wao kushindwa katika vita vya kwanza vya dunia.
Kando na ripoti za kuwepo mafuta na gesi katika ziwa hilo, ziwa lenyewe ni kivutio kikubwa cha watalii.
Malawi inasema inashauriana na Msumbiji kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika siku za baadaye ili kuzuia mzozo wa kidiplomasia .

Je hii ni mara ya kwanza kwa mzozo huu wa ziwa Malawi kutokea?

Hapana. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania.
Makubaliano hayo yaliafikiwa na Muungano wa Afrika na Tanzania ikaitikia ingawa shingo upande. Mzozo mpya kati ya nchi hizo ukaripotiwa tena kati ya mwaka 1967 na 1968.
Ulichipuka tena mwaka mwaka 2011, Malawi ilipotoa leseni ya kuchimba mafuta kwa kampuni ya British Surestream Petroleum Limited. Sehemu iliyotolewa kwa uchimbaji wa mafuta ni sehemu yenye mraba wa kilomita 20,000 sehemu ambayo Tanzania inasema ni yake.
Vyombo va habari viliripoti mwezi Julai mwaka 2012 kuwa mitumbwi ya wavuvi na ya watalii kutoka Malawi ilivuka na kuingia upande wa Tanzania
Tanzania nayo ikasema kuwa ingetafuta ushauri kutoka jamii ya kimataifa ikiwa nchi hizo hazingeweza kusuluhisha mzozo huo zenyewe.

Hofu ya hatua za kijeshi

Hofu ya mzozo kutokota na kuwa mbaya zaidi ilijitokeza mwaka 2012 wakati Tanzania iliposema kuwa ingelinda mipaka yake na kuzingatia sheria za kimataifa.

Utata kuhusu hatima ya faru John Tanzania



Faru mweusiImage copyrightTHE ASPINALL FOUNDATION
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka maafisa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kutoa ufafanuzi kuhusu kuhamishwa kwa faru maarufu kwa jina la John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
Bw Majaliwa amewataka viongozi wa NCAA kuwasilisha kwake nyaraka zote zilizotumika katika kumuhamisha faru huyo kufikia Alhamisi.
Alisema ana taarifa kuwa faru huyo John alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti katika eneo Serengeti mnamo 17 Desemba, 2015.
"… mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200 ambapo mkapewa shilingimilioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100 nyingine baadaye," alisema Bw Majaliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania, Bw Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa zozote kumhusu faru huyo ambazo zimetolewa.
"Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,".
Bw Majaliwa pia alimsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili.
Kwa sasa, anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haiwezekani mtumishi awe anachunguzwa na Takukuru halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini," alisema.
Hifadhi ya Ngorongoro ndilo eneo pekee Tanzania ambapo faru wanapatikana kwa wingi porini, ndani ya kreta.
Inakadiriwa kwamba idadi ya faru katika hifadhi hiyo ni takriban 35

Friday, 2 December 2016

BREAKING NEWS!!!!!!!!!!! TRUMP WA ST FRANCIS UNIVERSITY  ATANGAZA TENA NIA YA KUGOMBEA URAISI 2016/2017.




Huyu ni kijana aliyewania Urais katika kipindi cha muhula uliopita na hakufanikiwa kupita katika kinyanng'anyiro hicho cha uraisi. Kwa sasa kaja kivingine akiwa ni mgombea pekee anayejulika na kukubalika na  wanafunzi wengi sana hapa chuoni kwa umahili wake katika siasa za hapa chuoni lakini hata hivo watu wameenda mbali zaidi na kumfananisha na Raisi mteule mpya wa Marekani sir Donald Trump. Wachambuzi wa kisiasa wanaojulikana ndani na nje ya chuo wanaona kuwa kutokana na uamuzi wa TRUMP WA SFUCHAS kutangaza nia ya kugombea uraisi kutaufanya uchaguzi huo kuwa mwepesi zaidi kuliko chaguzi zilizopita miaka ya nyuma. Mwandishi wetu alikutana na baadhi ya wanafunzi wachache na wengi wao wanamkubali na wanadai trump atapata ushindi wa kishindo rai yao kubwa ilikuwa kumtakia kila raheli katika uchaguzi unaofanyika wiki ijayo.

Wednesday, 9 November 2016

Matokeo Marekani 2016: Trump amshinda Clinton uchaguzi wa urais. Siri ya Ushindi iko hapa


Mshirikishe mwenzako
Hillary Clinton and Donald TrumpImage copyrightAP
Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.
Bw Trump alikuwa ameshinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.
Alikuwa ameshinda Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.
Kwa sasa Trump ana kura 265 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.
Lakini mgombea wa Republican Bw Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.
Chama cha Republican pia kimehifadhi wingi wa wabunge katika Bunge la Wawakilishi.
Donald Trump alipakia picha hii kwenye Twitter, yake, mgombea mwenza wake na jamaa na marafiki wakifuatilia matokeo New York.Image copyright@REALDONALDTRUMP / TWITTER
Image captionDonald Trump alipakia picha hii kwenye Twitter, yake, mgombea mwenza wake na jamaa na marafiki wakifuatilia matokeo New York.
Kama ilivyotarajiwa, Bw Trump ameshinda katika ngome za Republican katika majimbo ya Alabama, Kentucky, South Carolina, Nebraska, Indiana, West Virginia, Mississippi, Tennessee, Oklahoma na Texas, ABC News wanakadiria.
Bw Trump pia anakadiriwa kushinda Arkansas, Kansas, North Dakota, South Dakota, Montana na Wyoming.
Shirika hilo linakadiria Bi Clinton atashinda ngome za Democratic majimbo ya New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island na District of Columbia.
Mshindi anahitaji kupata kura 270 kati ya jumla ya kura 538 za wajumbe ndipo atangazwe mshindi.
Voters cast their votes during the US presidential election in Elyria, Ohio, on 8 November.
Image copyrightREUTERS
Upigaji kura umemalizika katika majimbo 39 na matokeo kamili yalitarajiwa mwendo wa saa 23:00 EST (04:00 GMT Jumatano - Saa moja asubuhi Afrika Mashariki), upigaji kura utakaomalizika Pwani ya Magharibi.

Matukio mengine makuu:

  • Bodi ya Uchaguzi Carolina Kaskazini imekubali kuongeza muda wa kupiga kura maeneo manane wilaya ya Durham ambapo kuna milolongo mirefu ya wapiga kura.
  • Mgombea wa Republican aliyeshindwa kwenye mchujo Marco Rubio amehifadhi kiti chake cha useneta Florida
  • Thamani ya pesa za Mexico, peso, imeshuka sana baada ya Trump kuonekana akiongoza Florida
  • Mtu mmoja alifariki kwenye ufyatulianaji wa risasi karibu na kituo cha kupigia kura jimbo la Azusa, California. Watu watatu walijeruhiwa.
Bw Trump, tajiri kutoka Manhattan, na Bi Clinton, anayetaka kuwa rais wa kwanza mwanamke Marekani, walipiga kura mapema Jumanne katika jiji la New York.
Bw Trump alizomewa alipofika kupiga kura yake Manhattan, akiandamana na mkewe, Melania, na bintiye, Ivanka.
Wawili hao wamekuwa wakifuatilia matokeo kutoka jiji la New York.
Hillary ClintonImage copyright@HILLARYCLINTON / TWITTER
Image captionClinton amepakia picha hii, pamoja na ujumbe wa shukrani kwa watu wote, licha ya matokeo ya usiku wa leo
Bi Clinton atahutubia wafuasi Javits Centre, Manhattan naye Bw Trump atahutubu katika hoteli ya Hilton Midtown.
Maafisa wa polisi zaidi ya 5,000 wametumwa jijini New York kuimarisha usalama.
Utafiti wa maoni wa baada ya upigaji kura, uliofanywa na ABC News, unaonyesha wapiga kura 61% hawampendi Bw Trump nao 54% ndio hawampendi Bi Clinton.
Mapema Jumanne, Bw Trump kwa mara nyingine alikataa kusema iwapo atakubali matokeo.
"Tutaangalia tuone vile mambo yatakuwa," aliambia Fox News, huku akidai kwamba kumekuwa na kasoro hapa na pale kwenye uchaguzi.
"Ninataka kila kitu kiwe wazi."
Katika baadhi ya vituo, mitambo ya kupigia kura ilifeli na kwingine kukawa na milolongo mirefu, lakini yalionekana kuwa matatizo ya kawaida.
Bw Trump, aliyezua utata kuhusu kuaminika kwa shughuli ya uchaguzi kwa kudai kura "zitaibwa" mapema, pia amewasilisha kesi ya dharura Nevada.
Maafisa wa Republican wamemshtaki msajili wa wapiga kura wilaya ya Clark, wakidai jimbo hilo lilifungua vituo vya kupigia kura muda mrefu kuliko inavyofaa.
Lakini jaji ameitupilia mbali kesi hiyo.
Kando na kura za urais, Wamarekani wamekuwa pia wakipiga kura za Maseneta, wabunge wa Bunge la Wawakilishi na Magavana.
Viti vyote 435 Bunge la Wawakilishi vilikuwa vinashindaniwa, na ABC News wanakadiria kwamba bunge hilo litabaki chini ya udhibiti wa Republican.
Lakini theluthi moja ya viti Seneti, ambao Republican wamekuwa wanaongoza, pia vinashindaniwa, na Democratic wanatumai wanaweza kudhibiti bunge hilo.
Jumla ya Wamarekani 45 milioni, idadi kubwa zaidi kuliko awali, walijitokeza kupiga kura mapema.
Bw Trump na Bi Clinton wanapigania kumrithi Barack Obama wa Democratic.
Rais Obama haruhusiwi kuwania kikatiba baada ya kuhudumu mihula miwili ya miaka minne.
Rais mpya ataapishwa tarehe 20 Januari 2017.