TUNAKUPATIA HABARI ZA BIASHARA MICHEZO AFYA SIASA NA BURUDANI NA MAHUSIANO TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KUPITIA 0657191827,0753127275,0789930603
Wednesday, 27 July 2016
MOYO TAJIRI.
Ilikuwa imetimia saa mbili na nusu, asubuhi moja ambayo ilikuwa busy mno katika hospitali ya wilaya ya Ilala Amana.
Mwanamke mmoja mwembamba kiasi, na mrefu wa wastani mwenye sura nzuri na ngozi iliyoonekana kukosa matunzo ambae kwa kumtazama alikuwa na umri kati ya miaka 27-30 aliingia ofisini kwangu kufunguliwa P.0.P kwenye mkono aliokuwa amevunjika.
Akanieleza kwamba anayo haraka kidogo na akaniomba kama ninaweza kumhudumia, kwani daktari wake amemueleza kwamba leo hatokuwepo hospitalini na binafsi ana haraka kidogo.
Kama maadili ya taaluma yangu, sikutaka kumkasikirikia mgonjwa nikamuonyesha ishara ya kumruhusu kukaa.
Nikamuona mara kwa mara akitizama saa aliyokua amevaa mkono mwingine, nilitizama P.O.P na kumuelekeza akae mahala pengine ambapo ningeanza kazi ya kuondoa lile "hogo". Niliagiza Nesi aniletee vifaa vinavyohitajika. Aliniletea na nikaanza kazi.
Tukaanza kuongea mambo mbalimbali huku nikiendelea kumhudumia. Nikamuuliza kwanini anaonekana na haraka kiasi kile?
Mwanamke akanijibu kwamba anatakiwa kuwahi nyumbani akaandae chakula cha mume wake. Nikajiuliza ndio hilo tu lilimfanya anipelekeshe hvyo?
Kabla sijamueleza hilo akaendelea kuniambia kwamba mumewe ni mgonjwa na amepooza mwili mzima. Hii ikanigusa moyoni na nikaacha kumhudumia anieleze vizuri.
Akaendelea kuniambia kwamba mumewe amekuwa kitandani hajiwezi mwaka wa tano huu, alipatwa na maswahibu hayo mwaka mwaka mmoja tu tokea wafunge ndoa yao takatifu.
"Mume wangu yupo kitandani hajiwezi, hajui chochote kinachoendelea ulimwenguni kwani fahamu zake pia zimepotea! Ni mtu wa kutizama tu juu, haongei, hacheki bali machozi tu ndio humtoka.
"Ninampenda sana mume wangu, bado ninaimani ipo siku atakuja nyanyuka nikaliona tabasamu lake, kamwe siruhusu uoga wangu uharibu imani juu ya Mungu wangu"
"Maisha yamekua magumu sana, mume wangu anahitaji gharama nyingi kumhudumia, alikuwa na kazi nzuri sana na marafiki wengi, ila marafiki wote wamempa kisogo, walionekana mwanzoni tu alipopatwa na matatizo ila sasa siwaoni tena. Mzigo wote umekuwa wangu"
"Huu mkono nilivunjika katika Vilima vya Kimara Bonyokwa nilikokua nimetoka kuteka maji. Sina msaada wowote, tunaishi kwa fedha ambazo tumeuza mali zetu mbalimbali, nazo zinaelekea kuisha kwa vile hatuna chanzo kingine"
Niliahidi mbele ya kasisi na kadamnasi kwamba nitakuwa na mume wangu David katika shida na raha, ahadi yangu niliiweka kifuani kwangu na siku zote nitaisimamia mpaka pale Mungu atakapotoa uamuzi wake"
Alimaliza kunielezea yule mwanamke huku akijifuta machozi kwa mkono mwingine.
Sikujua ilikuwaje ila na mimi nilijikuta nikitokwa na machozi, nilimhudumia ipasavyo na nikamuahidi kumtembelea mapema nyumbani tujue namna tunaweza kumsaidia mumewe kwa matibabu zaidi.
Alivyoondoka nilijiambia kwamba "Hii ndio aina ya mapenzi nayoyahitaji katika maisha yangu, mapenzi ya kweli sio sura nzuri au hali nzuri tu, mapenzi ya kweli ni kukubali kila hali ambayo mwenzako anakabiliana nayo.
"True love is neither physical nor romantic. True love is an acceptance of all that is, has been, will be, and will not be."
Baada ya saa zangu za kazi nilirudi nyumbani kwangu nikiwa nimeaminishwa kwamba kumbe mapenzi ya kweli bado yapo!
Mwanamke mzuri kama yule atashindwaje kuolewa na wanaume wengine, ila ameamua kuwa upande wa mume wake katika dhiki kuu kama hiyo!!?
Kweli nilijifunza kitu kipya, hivyo basi nikaamua ku share nanyi rafiki zangu!
1. Kiapo mbele ya kiongozi wa dini na Mungu ni lazima kitimilizwe!
2. Mpende sana mke/mme wako, huwezi jua atakuwa msaada wako ukipatwa na matizo.
3. Marafiki hupenda kufurahi na wewe wakati wa neema, ukipata matatizo hutawaona. Hivyo basi thamini muda wa mpenzi wako zaidi kuliko kutumia muda mwingi na marafiki.
4. Ukishikwa, shikamana na ukipendwa pendeka!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment