Tuesday, 16 August 2016


MAISHA SIO FAIR. UFANYAJE KUFANIKIWA?



Kuna mambo mengi yanaweza kuwa wazi kwa mabishano au majibizano. Ila wengi mnaweza weza kukubali kuwa maisha sio fair. Maisha sio fair kwa jinsi wewe unavyoweza kupata milo 3 kwa siku wakati kuwa watu 21,000 wanakufa kila siku kwa sababu ya njaa. Mashuleni madebe ya uchafu yamejaa chakula, na wakati huohuo watu wanachangisha hela zitumwe Somalia kupigana na njaa. Maisha sio fair kwa jinsi kila siku unapita na daladala kuelekea Posta na unapishana na ombaomba huyo huyo kila siku. Mwaka mmoja baadae umenunua gari na bado yule ombaomba yupo na nguo zake zilezile zimechakaa. Maisha sio fair kwa jinsi pesa na kujuana na watu flani zinavyoweza kukufikisha popote pale utakapo, iwe ni umaarufu au hata kazi japokuwa huna maarifa yaliyo bora kupita wengine. Inafurahisha sana kuona familia yenye pesa, watoto wenye akili sana, wazazi wanaojua vitu na watu wakubwa na hivyo wanaweza kuwapatia watoto elimu bora, kuingia vyuo bora duniani na vya gharama bila wasiwasi na kuwahakikishia ajira kupitia watu wanaowajua. Ila fikiria, hii ni fair kwa yule mtoto wa masikini, mwenye akili lakini aliye na wazazi wasiojua vitu au watu wanaoweza kuwasaidia watoto wao kufikia mafanikio?

Lakini japokua maisha yanaweza yasiwe fair, kuna vitu vitatu ambavyo kila mtu anavyo au anaweza kuwa navyo. Haijalishi kuwa ni tajiri au masikini, mtu mzima au mtoto, mwanaume au mwanamke, vitu hivi vitatu vipo kwa wote. Ni hivi vitu ambavyo vinafanya kila kukicha tusikie stori ambazo huonekana kama muujiza. Stori za kama jinsi Bakhresa alivyotoka kuuza viazi vya mviringo mpaka kuwa kati ya matajiri wakubwa Afrika. Stori za kama jinsi Steve Jobs alivyokabidhiwa na wazazi wake kwa watu wengine wamlee mara baada ya kuzaliwa, jinsi alivyoacha kusoma chuo akihofia gharama kubwa na mpaka alivyokuwa mwanzilishi ya kampuni ya Apple, kampuni ambayo imetuletea bidhaa kama Iphone na Ipad. Ni vitu gani hivi?

1. Imani
Kwanza napenda kubainisha kuwa nachoongelea hapa si dini. Nachoongelea hapa ni kuamini kwamba iwe jua au mvua, jambo flani litatimia kwako. Ni kuamini kuwa hakuna kinachoweza kukufanya usifikie ndoto zako kwa kuwa kwako wewe tayari zishatimia. Ni ile Imani ya kuamini wewe ni tajiri wakati una jelo uliyokopa kutoka kwa rafiki yako Juma, ni ile Imani ya kujua ipo siku moja utaheshimika kimuziki kama Diamond wakati una single 5 umeachia na hakuna iliyohit, ni ile Imani ya siku moja na wewe utatajwa sambamba na Ray Kigosi kama kati ya waigizaji bora nchini, wakati huu ni mwaka wa tatu upo chuo cha Sanaa Bagamoyo unahangaika kujua kuigiza (ndoto yako ikitimia usinywe maji mengi lakini). Ni ile Imani ambayo ukimuelezea mtu kitu unachotaka kufanikisha basi atakuona chizi. Imani hii kila mtu anaweza kuwa nayo kama akikitaka kitu flani kwa moyo wake wote. Na ni hii Imani inayomwezesha mtu wa hali duni, mwenye shida na matatizo kibao kuweza kufanya mambo makubwa. Hebu jiulize, ni nini kilichomfanya mtangazaji Millard Ayo atake kuacha masomo ya sekondari na kusomea utangazaji, kama sio Imani kuwa huko ndiko kutamfaa?

2. Bidii
Kwa bahati mbaya sana, hizi sio enzi za Musa ambapo imani yako inaweza kugawanya bahari ili watu wapite. Bidii ya wajenzi itawawezesha wajenge daraja kwa haraka ili watu waweze kupita. Kuwa na Imani pekee haitoshi. Unahitaji kutumia muda na kufanya kazi ili ndoto yako itimie. Inabidi uendelee kusonga mbele hata kama matatizo na majukumu mengineyo yamekuandama bila kusahau kuwa Juma anataka jelo yake aliyokukopesha. Inabidi ujifunze kutosikiliza maneno ya watu wanaokuambia ndoto zako hazina maana hivyo uachane nazo na kufanya mambo ya ‘maana’. Inabidi unaposhindwa ujiinue na kuendelea na safari yako kama kawaida. Aliyegundua balbu alijaribu zaidi ya mara 1000 kuitengeza akashindwa. Na bado akaendelea kujaribu mpaka akapatia. Sasa fikiria, ina maana huyu mtu angekata tamaa alipojaribu mara ya 900 basi leo tusingekuwa na balbu. Hayo ndio maajabu ya bidii, kitu ambacho wewe na mimi tunacho au tunaweza kuwa nacho. Na kutokana na

No comments: