Monday, 15 August 2016


Edgar Lungu ashinda uchaguzi wa urais Zambia


Mshirikishe mwenzako
Rais Edgar Lungu wa Zambia
Image captionRais Edgar Lungu wa Zambia
Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangazwa mshindi wa matokeo ya uchaguzi wa urais kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi.
Tume ya uchaguzi nchini Zambia imesema kuwa Lungu alijipatia asilimia 50.35 siku ya Alhamisi ,ikiwa imepita asilimia 50 inayohitajika ya kuzuia raundi ya pili kulingana na sheria mpya ya uchaguzi.
Mpinzani wake Hakainde Hichilemi alijipatia asilimia 47.67 ya kura.
Awali,chama chake cha UNPD kilijiondoa katika shughuli ya kuhakiki kura akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu.

Aboud Jumbe aaga dunia kigamboni jijini Dar es salaam.

Mshirikishe mwenzako
Tanzania
Image caption
 
Rais mstaafu wa awamu ya pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia Jumapili saa saba mchana nyumbani kwake katika kijiji cha Mji Mwema, eneo la kigamboni jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohamed Aboud, mwili wa Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye pia alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kusafirishwa Jumatatu kwa ndege kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maziko.
Bwana Mohamed Aboud amesema Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Migombani, Mkoa wa Mjini Maghrib mnamo saa saba za mchana. Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 96 alizaliwa June 14, 1920 huko Juba, Sudan Kusini.
Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kuhudhuria maziko hayo ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi .
Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar April 7, 1972 mara tu baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa visiwa hivyo Abeid Amani Karume. Hayati Aboud Jumbe alijiuzulu urais wa Zanzibar pamoja na nyadhifa nyingine za makamu mwenyekiti wa CCM na makamu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 30, 1984

Friday, 5 August 2016


Viongozi wakutana kujadili mgogoro wa Sudan Kusini


Mshirikishe mwenzako

Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Sudan Kusini salva KiirImage copyrightAFP
Image captionRais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir

Viongozi wa Kikanda kutoka Afrika Mashariki wanakutana katika kikao cha dharura jijini Addis Ababa, Ethiopia kujadili mzozo wa Sudan Kusini.
Marais hao kutoka mataifa wanachama wa IGAD watajadili kwa kina pendekezo la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika AU kutaka kutuma vikosi vya usalama baada ya kuzuka upya kwa mapigano kati ya majeshi ya serikali na vikosi vya aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Hayo yanajiri siku mbili tu baada ya Rais Salva Kiir kuwatimua kazi mawaziri, washauri na wabunge wote wanaoegemea mrengo wa Machar.

Thursday, 4 August 2016

FUATILIA HIKI KISA

Tahadhari Kwa Wakenya : Uchawi Ni Utumwa.


                             Na. THEOFLIDA  WA  YESU.
Naanza  kwa  kuwasalimu  kwa  JINA  LA  YESU. Jina  lililo  Kuu  kupita  majina  yote. 
 
Wiki  kadhaa  zilizo  pita, niliandika  waraka  wangu   kwa  watanzania  na  kuusambaza   kupitia  blogs  na  mitandao  mbalimbali   kuhusu  athari  za  kujihusisha  na  masuala  ya  waganga  wa  jadi  . 

Katika waraka  huo   niliwatahadharisha  watanzania  kutojihusisha  na  WAGANGA  WA  TUNGULI  kwa  sababu WAGANGA  WA  TUNGULI  ni   WACHAWI NA MAWAKALA  WA  SHETANI   walio  vaa  kofia  ya  utabibu.

KUUSOMA  WARAKA  HUO, TAFADHALI  TEMBELEA 

:http://shuhudazaajabu.blogspot.co.ke/2016/07/ushuhuda-nilimlisha-mume-wa-mtu.html
 
  AU
 http://www.mpekuzihuru.com/2016/07/ushuhuda-nilimlisha-mume-wa-mtu.html
 
Katika  waraka  huo  niliwaelezea  watanzania  jinsi  nilivyo  shawishika  kutafuta  msaada  wa  maisha  yangu   kwa  MGANGA  WA  TUNGULI  aitwae  MUNGU  WA  KABILI  na  kujikuta  nikipata  matatizo  makubwa  ambayo  hata  hivyo  yalipelekea  kunikutanisha  na  YESU  ambae  ameniokoa.

Katika  waraka  huo nili  sahau  kueleza  mambo  makuu  mawili yafuatayo:

Kwanza  nilisahau  kuweka  mawasiliano  ya   MUNGU  WA  KABILI   ayatumiayo pindi  anapokuwa  nchini  KENYA ili  kuwa  tahadharisha  wakenya  wasipige  namba  hiyo  wala  wasijaribu  kutafuta  msaada  kwenye  namba  hiyo, kwa  sababu  mtu  huyo  ni  WAKALA  WA  SHETANI  alie  jificha  kwenye  kivuli  cha  UGANGA...

Wengi  walio  jaribu  kutafuta  msaada  kwa  MUNGU  WA  KABILI  wamejikuta  wakiishia  kuunganishwa  na  UTAWALA  WA  KUZIMU  ambao  umewapelekea  kujikuta  katika  matatizo  makubwa  kama   niliyo  yapata  mimi.

Nimeona  vyema  kuwatahadharisha  wakenya, kwa  sababu  mungu  wa  kabili  hufanya  kazi  zake  Tanzania  na  Kenya.  Anapokuwa  Tanzania, namba  yake  huwa  ni  + 255  744  000  473  na  anapokuwa  Kenya , namba  yake  huwa  ni  + 254    704  71 61 59.
 
Hivyo  basi   Ndugu  zangu Wakenya , hii ni  tahadhari  yangu  kwenu. Nimeweka  namba  hizo  hapo  juu  kama  alama  ya  MPINGA  KRISTO  ambayo  watu  wote  wenye  hofu  ya  Mungu  wanapaswa  kuepukana  nayo..

Nimeongozwa  katika  namna  ya  rohoni, kuanza  kufanya  kampeni  ya  nguvu  dhidi  ya  roho  ya  kuhusudu  masuala  ya  UGANGA, UCHAWI  NA  USHIRIKINA  na  nitajikita  zaidi  katika  mapambano  dhidi  ya  MGANGA  WA  JADI  AITWAE  MUNGU  WA  KABILI.
 
Ninaanza  kwa  kupambana  na  MUNGU  WA  KABILI  kwa  sababu, kwa  miaka  zaidi  ya  mitatu  ambayo  nimekuwa  nikishirikiana  na  MUNGU  WA  KABILI,  nimeweza  kujua  kuwa  yeye    ndio   MKUU  WA  WAGANGA  NA  WACHAWI  WOTE  WA  AFRIKA  MASHARIKI  NA  KATI , na  watu  wenye  hekima  wanasema  katikati  ya  kundi  la  kondoo  MPIGE  RUNGU  MCHUNGAJI, NA  KONDOO  WOTE  WATATAWANYIKA.

Naamini  nikimsambaratisha  mungu  wa  kabili, basi itakuwa  rahisi  kwa  waganga  wengine  kwa  sababu  wote  ni  kama  wafuasi  wake  tu.

Katika  kampeni  yangu  hii  ya  kiroho, nimeanzisha  blogu  iitwayo  SHUHUDA  ZA  AJABU  ambayo  inapatikana : www.shuhudazaajabu.blogspot.com.
 
Nitakuwa  nikitoa  shuhuda  za  mambo  mbalimbali  ya  kichawi  niliyo fundishwa  na  MUNGU  WA  KABILI  na  jinsi  unavyo  weza  kujiepusha  nayo  kwa  kutumia  Jina  la  Yesu.

Najua  kazi  hii  itainua  uadui  mkubwa  dhidi  yangu, kwa  sababu  hakuna  kitu  wachawi  wanakichukia  kama siri  zao  kutolewa  hadharani, lakini  kwa  Jina  la  Yesu, nitapambana  vita  hii  na  nitaishinda.
 
 MUNGU  WA  KABILI  na  jeshi  lake  watajaribu  kushindana  na  mimi  lakini  hawatashinda.( YEREMIA 1:19.)
 
Shuhuda  nitakazo  zitoa, zitakuwa  na  mafundisho  mazuri yatakayo  kupa  faida  , kama  Mungu  anavyo  sema katika  kitabu  cha ISAYA  48  kwamba  " MIMI  NI  MUNGU  NIKUFUNDISHAE  ILI  UPATE  FAIDA'.

Ushuhuda  huu  utakufanya  umjue  shetani  vizuri kama  wasemavyo  watu  wenye  hekima  " MJUE  ADUI  YAKO  KAMA  UNAVYO   IJUA  NAFSI  YAKO"

JAMBO  LA  PILI  na  la  msingi  ambalo  sikuweza  kuli

Sunday, 31 July 2016

JE UKO TAYARI KWA HILI?





"Je utakubali kuolewa na mimi?"
Akamuuliza mpenzi wake ambae ni mtarajiwa wake katika ndoa.
Mwanamke akainua kinywa chake kutaka kuzungumza lakini mwanaume akamzuia na kumwambia yafuatayo;
Akamwambia kabla hujanipa jibu lako, naomba uelewe kabisa ni nini nachokimaanisha na nini haswa kipo katika mahusiano ya ndoa.
Niwe mkweli kwako;
Ninakuomba uje kuwa mke wangu wa ndoa, katika Ndoa mapenzi huwa ni daraja jingine kabisa maana huko kuna nafasi nyingi zaidi za kuonesha upendo kati yetu.
Nitakufanya kama malkia wangu, nitakupenda siku zote, na utakuwa kipaumbele changu.
Mwanaume akamshika mkono mwanamke wake na kuendelea kumwambia, "Lakini unapaswa kutambua kwamba katikati ya ndoa yetu kutakua na misuguano na mikwaruzano ya hapa na pale, mimi sio mkamilifu asilimia 100.
Ninaweza nikakuudhi mara kadhaa, ninaweza kukusababishia hasira, haijalishi ni kiasi gani nitakukosea naomba tu utambue kuwa kukusoma na kukuelewa wewe ni somo endelevu.
Mimi na wewe tumekutana ukubwani, tumelelewa katika familia tofauti. Lazima tu nitakuwa na baadhi ya vitu usivyovipenda. Nivumilie!
Ndio maana siku zote namuomba Mungu azidi kunifunza kukupenda wewe!
Mwanamke akamtizama mwanaume wake kwa macho ya upendo!
Mwanaume akaendela, "vitu vingi sana utavitarajia kwangu nikiwa kama mume wako. Nitakuwa kichwa cha nyumba, nitahitajika kutunza familia na kuiongoza vema, lakini lazima kutakuwa na siku njema na mbaya.
Katika siku mbaya, nifariji, nipe moyo, niamini mimi, nikumbatie na uwe nguzo yangu. Nitafute pale nitakapopotea, nisamehe pale nitakapokosea.
Lakini kama unaona nakuomba vitu vingi basi usikubali kuolewa na mimi. Nataka niwe mkweli kwako kabla hatujaingia katika Ndoa.
Mwanamke akamkisi mwanaume wake katika paji la uso na kumwambia yafuatayo;
"kabla sijakubali proposal yako ya kunioa naomba na mimi niwe mkweli kwako. Nakupenda na ninafahamu ni nini maana ya upendo.
Upendo hauhesabu mabaya, upendo husamehe, upendo huvumilia. Ningeweza kuwa single maisha yangu yote lakini sicho kitu ambacho nilikihitaji.
Ninachokihitaji ni wewe tu!
Nahitaji mapenzi kutoka kwako, nitakupenda hata kipindi kibaya katika maisha. Nina moyo ambao umejazwa upendo, na ninahitaji sana niutumie kwako."
Mwanamke akamtizama mwanaume wake na kuendelea kumwambia;
"Ninakupenda jinsi ulivyo, mali na fedha tutazitafuta pamoja furaha na amani niliyonayo ni mtaji tosha.
Nafurahi kwa kuwa umesema utajifunza kuishi na mimi, basi nami pia nitajifunza kuishi na wewe.
Katika ndoa, naweza nikasema mambo ya kuudhi na kufanya yale ya kuudhi, naweza nikawa sina mood muda mwingine, naweza nikawa nimechoka, na kuhitaji muda kidogo peke yangu. Hiyo haitamaanisha sikupendi tena la hasha ni darasa tu la kujifunza kuishi pamoja."
Muda mwingine naweza nikahangaika kubalance kuwa mke, mama, binti wa wazazi wangu, mfanyakazi ofisini na dada wa ndugu zangu, naomba nivumilie kwa hilo na unielewe pia."
Nipende, nijali, niheshimu, nivumilie hata pale nitakapovaa gauni la ujauzito kama Mungu akitujaalia, nami nitakupenda siku zote."
Mwanamke akafumba macho na kufungua kuendelea kuongea "itakuwa ndoto yangu imekamilika kuishi na wewe, mfalme wangu. Mwalimu wangu na mwanafunzi wangu vilevile. Sihitaji kuwa peke yangu, nahitaji kuwa na wewe.
Nahitaji kuwa mke mwema kwako.
Kwa kujiamini kabisa nakujibu Ndio nitakubali kuolewa na wewe"
Share
Weekend njema.
Tweve

Thursday, 28 July 2016


UN yaitupia lawama Boko Haram

Mshirikishe mwenzako
Image copyrightAFP
Umoja wa Mataifa umelilaumu kundi la itikadi kali la Boko Haram kwa ghasia ambazo imeziita zisizoeleweka na ukatili nchini Nigeria
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja huo Stephen O'brien amesema hatua za kundi hilo zimefanya idadi kubwa ya watu kuyakimbia makaazi yao.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu milioni tisa wamevuka bonde la mto Chad na kuelekea maeneo mengine ya Nigeria, Niger, Chad na Cameroon kwa lengo la kutafuta msaada wa kibinadamu

Wednesday, 27 July 2016


MOYO TAJIRI.



Ilikuwa imetimia saa mbili na nusu, asubuhi moja ambayo ilikuwa busy mno katika hospitali ya wilaya ya Ilala Amana.
Mwanamke mmoja mwembamba kiasi, na mrefu wa wastani mwenye sura nzuri na ngozi iliyoonekana kukosa matunzo ambae kwa kumtazama alikuwa na umri kati ya miaka 27-30 aliingia ofisini kwangu kufunguliwa P.0.P kwenye mkono aliokuwa amevunjika.
Akanieleza kwamba anayo haraka kidogo na akaniomba kama ninaweza kumhudumia, kwani daktari wake amemueleza kwamba leo hatokuwepo hospitalini na binafsi ana haraka kidogo.
Kama maadili ya taaluma yangu, sikutaka kumkasikirikia mgonjwa nikamuonyesha ishara ya kumruhusu kukaa.
Nikamuona mara kwa mara akitizama saa aliyokua amevaa mkono mwingine, nilitizama P.O.P na kumuelekeza akae mahala pengine ambapo ningeanza kazi ya kuondoa lile "hogo". Niliagiza Nesi aniletee vifaa vinavyohitajika. Aliniletea na nikaanza kazi.
Tukaanza kuongea mambo mbalimbali huku nikiendelea kumhudumia. Nikamuuliza kwanini anaonekana na haraka kiasi kile?
Mwanamke akanijibu kwamba anatakiwa kuwahi nyumbani akaandae chakula cha mume wake. Nikajiuliza ndio hilo tu lilimfanya anipelekeshe hvyo?
Kabla sijamueleza hilo akaendelea kuniambia kwamba mumewe ni mgonjwa na amepooza mwili mzima. Hii ikanigusa moyoni na nikaacha kumhudumia anieleze vizuri.
Akaendelea kuniambia kwamba mumewe amekuwa kitandani hajiwezi mwaka wa tano huu, alipatwa na maswahibu hayo mwaka mwaka mmoja tu tokea wafunge ndoa yao takatifu.
"Mume wangu yupo kitandani hajiwezi, hajui chochote kinachoendelea ulimwenguni kwani fahamu zake pia zimepotea! Ni mtu wa kutizama tu juu, haongei, hacheki bali machozi tu ndio humtoka.
"Ninampenda sana mume wangu, bado ninaimani ipo siku atakuja nyanyuka nikaliona tabasamu lake, kamwe siruhusu uoga wangu uharibu imani juu ya Mungu wangu"
"Maisha yamekua magumu sana, mume wangu anahitaji gharama nyingi kumhudumia, alikuwa na kazi nzuri sana na marafiki wengi, ila marafiki wote wamempa kisogo, walionekana mwanzoni tu alipopatwa na matatizo ila sasa siwaoni tena. Mzigo wote umekuwa wangu"
"Huu mkono nilivunjika katika Vilima vya Kimara Bonyokwa nilikokua nimetoka kuteka maji. Sina msaada wowote, tunaishi kwa fedha ambazo tumeuza mali zetu mbalimbali, nazo zinaelekea kuisha kwa vile hatuna chanzo kingine"
Niliahidi mbele ya kasisi na kadamnasi kwamba nitakuwa na mume wangu David katika shida na raha, ahadi yangu niliiweka kifuani kwangu na siku zote nitaisimamia mpaka pale Mungu atakapotoa uamuzi wake"
Alimaliza kunielezea yule mwanamke huku akijifuta machozi kwa mkono mwingine.
Sikujua ilikuwaje ila na mimi nilijikuta nikitokwa na machozi, nilimhudumia ipasavyo na nikamuahidi kumtembelea mapema nyumbani tujue namna tunaweza kumsaidia mumewe kwa matibabu zaidi.
Alivyoondoka nilijiambia kwamba "Hii ndio aina ya mapenzi nayoyahitaji katika maisha yangu, mapenzi ya kweli sio sura nzuri au hali nzuri tu, mapenzi ya kweli ni kukubali kila hali ambayo mwenzako anakabiliana nayo.
"True love is neither physical nor romantic. True love is an acceptance of all that is, has been, will be, and will not be."
Baada ya saa zangu za kazi nilirudi nyumbani kwangu nikiwa nimeaminishwa kwamba kumbe mapenzi ya kweli bado yapo!
Mwanamke mzuri kama yule atashindwaje kuolewa na wanaume wengine, ila ameamua kuwa upande wa mume wake katika dhiki kuu kama hiyo!!?
Kweli nilijifunza kitu kipya, hivyo basi nikaamua ku share nanyi rafiki zangu!
1. Kiapo mbele ya kiongozi wa dini na Mungu ni lazima kitimilizwe!
2. Mpende sana mke/mme wako, huwezi jua atakuwa msaada wako ukipatwa na matizo.
3. Marafiki hupenda kufurahi na wewe wakati wa neema, ukipata matatizo hutawaona. Hivyo basi thamini muda wa mpenzi wako zaidi kuliko kutumia muda mwingi na marafiki.
4. Ukishikwa, shikamana na ukipendwa pendeka!